Ujumbe wa Papa kwa maadhimisho ya Siku Kuu ya Bikira Maria wa Upendo wa Cobre Cuba.
Jumamosi, Baba Mtakatifu Francisko alituma ujumbe wake kwa Askofu Mkuu Dionisio Guillermo
García Ibáñez, wa Jimbo Kuu la Santiago de Cuba, ambaye pia ni Rais wa Baraza la
Maaskofu Katoliki Cuba, kwa ajili ya sherehe ya kitaifa ya kuienzi sanamu ya Bikira
Maria wa Upendo wa Cobre hapo tarehe 8 Septemba, ambayo nakala yake imewekwa pia
katika Bustani za Vatican. Katika ujumbe huo Papa amesema, uwepo wake sanamu hiyo
katika Bustani za Vatican, ni kumbukumbu inayoamsha hisia katika uhai wa Kanisa linalosafiri
katika nchi za Caribbean kwa zaidi ya karne nne, ambalo kwa mara nyingine linakusanyka
tena mbele ya Sura ya Mama wa Mungu, Mpendevu. Na sasa ni kutoka milima ya El Cobre,
hadi kwa Khalfa wa Mtume Petro. Wana heri wale wanaopata muda hata kidogo wa kusimama
katika madhabahu haya ya Maria, na kufanya ibada ya kuomba msaada wa kuongozwa nae,
kumwelekea Yesu, Mwana wake. Papa Francisco anaaendelea kusema, leo hii, kwa bidii
tunaisherehekea Sikukuu hii ya Maria, Bikira wa "Mambisa," ambaye Wacuba wote, wameyageuza
macho yao kwa Moyo wake Safi, kumwomba neema. Kwa ajili hiyo Papa, ametoa pongeza
kwa wapendwa hao wote, huku akiwataka waige unyenyekevu wake na uaminifu wake kwa
Kristo, ambavyo sharti la kwanza la mwanafunzi bora wa Yesu. Na kwamba, yeye Papa
kila mara anaposoma maandiko matakatifu, ambamo Bwana anaongea na anaongea ya Mama
yetu, hupatwa na mawazo katika maneno matatu: shangilia, uamka na uvumilia. Papa
ameelezea kushangilia, akisema lilikuwa ni neno la kwanza la Malaika Gabriel kwa Bikira
Maria, “Salaam, umejaa neema, Bwana yu pamoja nawe" (Lk 1:28).Na hii inaonyesha maisha
ya mtu aliyemgundua Yesu, ni kujazwa na furaha ndani, kwamba hakuna kitu chochote
na hakuna mtu anaweza kuinyakua furaha hiyo. Na ndivyo ilivyo kwa Wakristo wa Cuba
katika Siku Kuu hii, wanafurahi kwa sababu ya kuwa ya uwepo wa Bikira wa Upendo,
anayetoa mwaliko kwa watu wote, kuishi kwa upendo wa kweli, na si kuanguka katika
mitego mibovu ya maisha ya jicho kwa jicho - jino kwa jino. Ni furaha iliyoje kusikia
yupo mmoja mwenye kuwa na upendo wa kweli, pamoja na ukweli wa maisha, na si ya wale
wenye kutoa maneno matupu, yenye kupeperushwa mbali kwa upepo. Papa pia amelizungumzia
neno la pili, amka akirejea Injili ya Mtakatifu Luka, ambamo Maria aliamka na kwenda
kumsaidia binadamu yake Elizabeth, ambaye katika uzee wake alikuwa akisubiri kuzaa
mtoto (Luka 1: 39-45). Hii ilikuwa ni kutimiza mapenzi ya Mungu, kwa wale wanaohitaji.
Maria alifikiria juu ya matatizo ya wengine na kujitolea kuwasaidia. Huu ni ushindi
mwingine wa Maria, ananyanyuka na kwenda kusaidia mhitaji. Na ndivyo nasi pia tunahitaji,
kuwa tayari kusaidia wahitaji wenye shinda. Tunahitaji kumwiga Maria bila kukata tamaa
katika kuubeba mzigo wa wengine kama wajibu wetu. Na haya si mambo makubwa,iwapo
tutafanya hivyo kwa upendo unaotoka ndani ya maisha yaliyobadilishwa na Yesu, kufanya
kila kitu kwa huruma. Maria daima anafanya hivyo, yuko karibu na watu wake, katika
neema ya watoto. Yeye aujua upweke, umaskini na hata maisha ya uhamishoni, na amejifunza
jinsi ya kujenga udugu na kufanya sehemu yoyote, kuwa mahali pazuri pa kukaa. Na tumwombe
atupe roho ya mtu maskini ambaye hana kiburi, moyo safi wenye kumcha Mungu, bila
kurudishwa nyuma na ugumu wa maisha. Na neno la tatu ni tumaini. Maria, ambaye
ana uzoefu wa wema wa Mungu, alitangaza ukuu kwamba alio mfanyia (Luka 1, 46-55).
Maria hakuzitumainia nguvu zake mwenyewe, lakini katika Mungu, ambaye upendo wake
hauna mwisho. Kwa hili, alibaki na Mwanae , na Mitume wake bila kupoteza tumaini.
(Matendo 1:14). Na ndivyo nasi pia tunaitwa kubaki katika upendo wa Mungu na kukaa
katika upendo wa wa kuwaelekea wengine, katika dunia hii yenye matatizo mengi, bila
ya kupoteza tumaini. Papa alikamilisha ujumbe wake kwa kuwataka wana wa kanisa Cuba
pia wamkumbuke katika sala zao.