Papa: hakuna sababu za kuhofia mabadiliko katika Kanisa
Papa Francisco mapema Ijumaa alitoa wito kwa waumini wote kutohofia mabadiliko ndani
ya Kanisa, kwa kuwa, ujumbe wake wa Injii ni habari njema, ambamo Yesu anatutaka
kuachana na miundo ya maisha isiyofaa tena. Papa alitoa rai hiyo wakati akiongoza
Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta la ndani ya Vatican.
Alisema
kuwa, Mkristo hapaswi kuwa "Mtumwa wa sheria nyingi ndogo ndogo ", lakini ni kuufunua
moyo wake kwa amri mpya ya upendo. Papa alisema hilo kwa kutazama unafiki wa waandishi
mafarisayo, walivyofikiri wanaweza kumdhihaki Yesu kwa kumwuliza maswali kwa kejeli
kama kwa nini wanafunzi wake hawafungi. Lakini Bwana alitambua hilo na kuwapa majibu
yaliyowafanya watazame chini kwa aibu.
Papa pia alifafanua ujumbe wa Injili
katika mfano wa “Mvinyo mpya, viriba vipya” akisema, hii ni habari ya furaha kwamba,
walimu hawa wa sheria walikuwa wamefungwa katika amri za maagizo yao. Hata Mtume Paulo
anasema, kabla ya ukombozi wa Yesu, wote walikuwa wafungwa chini ya sheria. Papa
alisema, sheria za watu hao si kwamba zilikuwa ni mbaya, zilisaidia kuwalinda, lakini
kwa kuwaweka kama wafunga wa sheria katika mtazamo wa imani. Sheria nyepesi ya
Yesu ya Upendo, iliweza kuwafungua waumini dhidi ya sheria hizo nyinginyingi. Imani
iliyowekwa wazi zaidi na Yesu mwenyewe.
Papa alieleza na kuhoji iwapo Ukristo
una sheria na alitoa jibu “Ndiyo”. Yesu alisema: 'Mimi sikuja kuifunga sheria, lakini
kuikamilisha katika ukamilifu wake. Na ukamilifu wa sheria, kwa mfano, umo katika
sheria ya Upendo na Heri za Mlimani,zilizotajwa na Yesu, na kama alivyotupenda. Na
wakati Yesu anawakemea walimu hawa wa sheria, ni kwa kuwa washindwa kuwasaidia watu
kuzielewa sheria badala yake waliwafanya kuwa watumwa wa sheria nyingi, katika mambo
madogo madogo mengi, yakiwa si ya lazima kufanya hivyo.
Na sasa nini cha
kufanya, aliongeza, kwa uhuru ulioletwa na Yesu, unatuongoza katika ukamilifu wa
sheria yake mpya, sheria aliyoikamilisha kwa damu yake mwenyewe. Na hili ni upya
wa Injili, yenye kutupa mpumuo wa furaha ya kweli na uhuru. Na ndiyo maana ya mvinyo
mpya na na viriba vipya. Na hivyo tusiwe na woga wa kufanya mabadiliko kwa mujibu
wa sheria ya Injili.
Papa Francisco mapema Ijumaa hii alitoa wito kwa
waumini wote kutohofia mabadiliko katika Kanisa, kwa kuwa Injii ni Ujumbe , na Yesu
anatutaka kuachana na miundo isiyofaa tena. Papa alitoa rai hiyo wakati akiongoza
Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta la ndani ya Vatican. Papa
alisema kuwa, Mkristo hapaswi kuwa "Mtumwa wa sheria nyingi ndogo ndogo ", lakini
ni kuufunua moyo wake kwa amri mpya ya upendo. Papa alisema hilo kwa kutazama jinsi
Waandishi mafarisayo walivyofikiri wanaweza kumdharirisha Yesu kwa kumwuliza maswali
magumu kama kwa nini wanafunzi wake hawafungi. Lakini Bwana anatambua mtego wao na
kuwapa majibu yaliyowafany akwatazame chini kwa aibu. Papa pialaifafanua ujumbe
wa Injili katika mfano wa “Mvinyo mpya, viriba vipya” ulioandikwa katika Injili akisema,
hii ni habri ya furaha kwamba, walimu hawa wa sheria walikuwa wamefungwa katika amri
za maagizo yao. Hata Mtume Paulo anasema, kabla ya ukombozi wa Yesu, wote walikuwa
wafungwa chini ya sheria. Papa alisema, sheria za watu hao si kwamba zilikuwa ni mbaya,
ziliwalinda lakini kwa kuwaweka kama wafunga katika mtazamo wa imani. Imani hiyo iliyowekwa
wazi zaidi na Yesu mwenyewe.
Papa alieleza na kuhoji iwapo Uristo hauna sheria
na alitoa jibu la “Ndiyo”. Yesu alisema: 'Mimi sikuja kuifunga sheria, lakini kuikamilisha
katika ukamilifu wake. Na ukamilifu wa sheria, kwa mfano, ni Heri alizohubiri Yesu
Mlimani, sheria ya upendo, upendo jumla, kama Yeye - Yesu - alivyotupenda. Na wakati
Yesu anawakemea watu hawa, hawa madaktari wa sheria, sanawakemea kwa kushindwa kuwasaidia
watu kuzielewa sheria badala yake wanawafnya kuwa watumwa wa sheria nyingi katika
mambo madogo madogo mengi, yakiwa si ya lazima kufanya hivyo. Na sasa nini cha
kufanya, aliongeza, ni kwa uhuru ulioletwa na Yesu unaotuongoza katika ukamilifu
wa sheria yake mpya, sheria aliyoikamilisha kwa damu yake mwenyewe. Na hii ni upya
wa Injili, yenye kutupa mpumuo wa furaha ya kweli na uhuru. Na hivyo ndiyo maana
ya mvinyo mpya na na viriba vipya. Na hivyo tusiwe na woga wa kfuanya mabadiliko kw
amujibu wa sheria ya Injili.