2014-09-06 09:18:44

Decania ya Makardinali yaiombea Roho ya Marehemu Kardinali Szoka ..


Kardinali Angelo Sodano, Mkuu wa Dekania ya Makardinali, Alhamis Septemba 4,aliongoza Ibada ya Misa, katika Kanisa dogo linalotumiwa mara kwa mara na maafisa wa utawala wa Vatican, kwa nia ya kuiombea roho ya Marehemu Kardinali Edmund Casimir Szoka, aliyefariki Agosti 20, 2014.

Kardinali Angelo Sodano katika mahubiri yake alisema, ilikuwa ni wajibu kukutana katika Ibada na kutolea shukurani zao kwa pamoja karibu na madhabahu ya Bwana, kuiombea roho ya marehemu Kardinali Edmund Casimir Szoka, aliye tulia katika ukimya wa milele usiku, Agosti 20, kati ya kuta za hospitali katika nchi yake pendwa ya Marekani, akiwa na umri wa 8. Roho yake ilirudi kwa Mungu, Muumba wake, kwa jina la Mwanawe alimkomboa na katika jina la Roho Mtakatifu alimweka wakfu.

Marehemu katika miaka yake ya mwisho 17 alilitumikia Jimbo Kuu la Detroit, kama mchungaji wake aliyelitumikia Kanisa Kuu la Sakramenti Kuu Takatifu Sana, hadi Agosti 26 mwaka jana.Na pia alikwa kipindi cha miaka 16 ya utumishi wake wa kichungaji , alifanya kazi kwa ukaribu sana na Papa John Paul II, kwanza katika masuala ya Uchumi ya Jimbo Takatifu, na kisha kama Rais wa Utawala Vatican.

Kardinali Angleo Sodano aliendelea kusema, ni wajibu na haki, kuungana na jamii hasa waliokuwa chini Mchungaji huyu mwaminifu, Marekani na Vatican, kukiomboleza kifo cha kiongozi huyu wa kanisa mbele za Bwana. Na pia ni wajibu na haki kuyakumbuka maisha yake ya majitoleo kwa ajili ya huduma ya kanisa , akiwa tayari hata kuiacha nchi yake pendwa na kuja Roma kuhudumia Kanisa la Ulimwengu kwa moyo wa huduma, busara na utulivu katika Kiti Kitakatifu cha Khalifa wa Mtume Petro.
Kardinali baada ya kutoa ufafaunzi kwa masomo ya siku, alitoa mwaliko kwa wote waliohudhuria Ibada hiyo, kusali pamona ili kwamba katika Bwana, mwanga wa amani, uambatane na ndugu yetu marehemu Kardinali Szoka,na kutuongoza sisi pia, ili siku moja tuweze kurudia maneno ya Mzee Simeoni: "Sasa Bwana, wamruhusu mtumishi wako aende kwa amani, kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako "(Luka 2, 29-30).
All the contents on this site are copyrighted ©.