2014-09-05 08:14:04

Ujumbe wa Papa kwa Wakristo wanaoteseka :Kanisa li pamoja nao


Jumatano, Baba Mtakatifu Francisco, akitoa katekesi yake kwa mahujaji wageni, aliwakumbuka pia Wakristo wanaoteseka kwa sababu ya imani yao kwa Kristo, hasa nchini Iraki kwa wakati huu. Aliwatia moyo Wakristo akiwahakikishia kwamba, Kanisa ni Mama yao na huonea fahari kuwa na watoto kama wao. Papa alielezea umama wa Kanisa akimtafakari Mama Bikira Maria, ambaye anakubali kulibeba Kanisa, kulipenda na kuwatetea watoto wake, dhidi ya madhulumu na madhara.

Papa aliendelea kutaja jinsi Kanisa linavyojivunia na kuona fahari ya kuwa na jumuiya aminifu ya waamini ambao hawafichi imani yao kwa Kristo mbele ya huyo anayebisha mlango akiwa na bundukitayari kuwamaliza. pia linavunia wale wanao endelea kwenda katika ibada za Misa huku wakijua hatari za uwepo wa mabomu.

Papa Francisko aliizungumzia mada hii ya Mama Kanisa kwa sauti ya nguvu, isiyokuwa na woga katika kuwatetea wana wa kanisa wa Iraki na wote wanaopambana na madhulumu kama haya ya mauaji ya watu wasiokuwa na hatia ila kwa sababu ya wogofu wao kwa Kristo.
Alisema, “nataka kuwahakikishia, na hasa yale yanayo tokea hivi sasa kwamba, wanyonge wasioweza kupambana kwa silaha, na wakimbizi , ninyi nyote mko ndani ya moyo wa Kanisa; Kanisa linateseka pamoja nanyi na linaona fahari kuwa nanyi kama wana wa Kanisa. Ninyi ni nguvu za Kanisa na mashahidi shupavu wa ujumbe wa kuokoa ,msamaha na upendo. Mimi namkumbatia kila mmoja ndani ya moyo wa wangu! Bwana awabariki na kuwalinda siku zote".

Maelezo haya ya Papa yalitiwa ladha zaidi na msisitizo kwamba, haiwezekani kuwa Mkristo wa kweli kwa kujitenga na wengine, au kwa juhudi binafsi na kwamba ukristo hautengenezwi au kuunda ndani ya karakana au maabara, lakini ni ndani ya mwili unaolishwa na Neno la Mungu. Mama Kanisa hulisha wana wake kwa Neno la Mungu. Ni tu kwa kulisiliza Neno la Mungu na kuliamini, tunapata nguvu ya mabadiliko katika maisha yetu, mabadiliko yanayokea ndani ya moyo.

Papa alisisitiza , kila Mkristo, anaitwa kuishuhudia imani yake kwa Kristo kwa ujasiri wa kimama, na kuzikataa hali zote za woga kwa sababu kuwa Mkristo ni tofali katika mwili wa Kanisa ambao ni upendo, msahaha na wokovu. Na kwamba Kanisa si Maaskofu au Mapadre au watawa, la hasha, Kanisa ni waamini wote wanaomkiri Kristo. Na hivyo wote hao ni wana wa Mama Kanisa.







All the contents on this site are copyrighted ©.