Papa akutana na Shimon Peres na Mwana Mfalme wa Jordan
(Vatican Radio) Papa Francisko, AlhamIsi asubuhi, alikutana katika mazungumzo ya faragha
na watu mashuhuri wawili, Rais wa zamani wa Israeli, Shimon Peres, na mwingine Mwana
Mfalme El Hassan bin Talal wa Jordan. Padre Federico Lombardi, SJ, Mkurugenzi
wa Ofisi ya Habari Vatican, aliwapa taarifa fupi wanahabari kwamba, Rais wa zamani
Peres aliomba kukutana na Papa hasa kwa ajili ya kumfahamisha Papa shughuli zake
na miradi yake kwa ajili ya amani, ikiwemo mpango wa pamoja wa kuwashirikisha vijana
katika michezo katika miji ya Israel na Palestina, ambamo zaidi ya watoto themanini
watashiriki, katika nyakati mbalimbali kama itavyokuwa imeandaliwa mwaka kwa mwaka,
na taasisi ya muungano wa dini, iliyobuniwa na Umoja wa Mataifa. Akizungumza na
Radio Vatican baada ya mkutano huo,Padre Lombardi aliutaja mkutano wa Papa na Rais
wa zamani wa Israel kwamba ulidumu takribani dakika 45, na Papa alimsikiliza kwa makini
na kueleza mawazo yake pia juu ya mpango wa Rais Peres, na kumhakikishia kwamba Idara
husika za Curia ya Roma zitatoa ushirikiano wa hali ya juu, hasa zinazohusika na amani
na maridhiano kati ya tamaduni na dini mbalimbali, na hasa Baraza la Kipapa kwa ajili
ya Mazungumzo kati ya dini, na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki na Amani, na Makardinali
Tauran na Peter Turkson.
Kuhusu pendekezo la Rais wa zamani Peres, kuunda
Taasisi ya kuunganisha dini "United Religions", Padre Lombardi amesema ni mada iliyojadiliwa
katika mkutano wa viongozi hawa kwa makini, na pia ilikuwa kama nafasi ya kupitia
upya mkutano wa kihistoria katika Vatican, wakati Rais Peres na Rais wa Palestina
Mahmoud Abbas, waliposhiriki katika mkutano wa sala ya amani hapa Vatican, juhudi
ambazo haziwezi kutajwa kama zilishindwa kwa kuwa zinaendelea kufanyiwa kazi na hivyo
imekuwa kama ni kufungua mlango wazi, kwaajili ya kuanzisha juhudi mbalimbali katika
lengo hilo la ujenzi wa amani na maridhiano, kwa njia ambayo juhudi na maadili vinaweza
kuwa moyo wa kusonga mbele na hatua hizo, jambo lililosisitizwa na Papa Francisko
hata baada ya kukutana na Rais Peres.
Na juu ya Papa kukutana na Mwana Mfalme
Hassan wa Jordan, Padre Lombardi alieleza kwamba, ulikuwa ni muhimu pia na katika
mtazamo huohuo wa kuwasilisha kazi kuwasilisha kazi zaTaasisi yenye utendaji wenye
mwingiliano wa dini, tafiti za tamaduni na majadiliano iliyoanzishwa na Mwana Mfalme
ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza, pia kama ilivyo kwa Taaisisi ya Kifalme ya tafiti
kati ya dini mbalimbali , ambayo pia aliianzisha Mwana Mfalme Hassan. Shuguli za taasisi
hizo zote zimeelekezwa katika kufanikisha majadiliano kati ya dini na dhamira ya
amani, katika mazingira ya sasa ya vurugu. Na hivyo kunakuwa na umuhimu wa kipekee
kufanikisha majadiliano baina ya dini kwa heshima ya binadamu na amani, na kusaidia
masikini katika wakati wa utandawazi, elimu kwa vijana, ushirikiano katika udugu,
na msisitizo juu ya heshima na hadhi ya binadamu wote.
Aidha Padre Lombardi,
alitoa taarifa fupi juu ya safu ya mada nyingine, ikiwa ni pamoja na mkutano wa Baraza
la Uchumi la Vatican - uliofanyika Alhamisi, ili kuchunguza masuala ya kisheria,
kiufundi yanayohusiana na mageuzi ya taasisi Vatican kiutawala na ya kifedha - na
uwezekano wa mkutano kati ya gavana wa Usharika kwa Mafundisho ya Imani, Kardinali
Gerhard Mueller, na Mkuu wa Udugu wa Matakatifu Pius X, Askofu Bernard Fellay, ambao
tarehe yake bado kujulikana.