2014-09-04 08:22:33

Salaam za Papa kwa Mkutano wa Kimataifa wa Kiekumeni- Bose


Kwa ajili ya tukio la Mkutano wa 22 wa Kimataifa juu ya Roho ya Kiekumeni ya Kiotodosi, unao fadhiliwa na Jumuiya ya Bose pamoja na Makanisa Orthodox juu ya mada "Heri wenye kuleta amani", Baba Mtakatifu Francisko , amepeleka salaam zake za matashi mema kwa waandaaji na washiriki wa mkutano huo.

Papa katika salaam hizo zilizotiwa sahihi na kutumwa na Katibu wa Jimbo la Papa Kardinali Pietro Palorin, ametoa shukrani kwa uwepo wa mkutano huo. Na ameonyesha tumaini lake kwamba, siku hizi za tafiti na majadiliano, zitaweza kukuza uelewa kwamba inawezekana wabatizwa wote kuishi na kushuhudia amani iliyo tangazwa na Kristkw pamoja. Na kwamba udugu wa kweli hufifisha ugomvi, na kutoaminiana na badala yake huzaa matumaini. Baba Mtaktifu ametoa mwaliko kwa watu wote kutolea sala zao kwa ajili ya kazi za mkutano huu na kwa ajili ya utumishi wake kwa Kanisa. Mwisho ametoa baraka zake za kitume.








All the contents on this site are copyrighted ©.