2014-09-04 08:40:57

Mafundisho ya Kanisa juu ya heshima ya Kazi


(Vatican Radio) Katika Maadhimisho ya Kitaifa ya SIku ya Kazi Marekani, Askofu Mkuu Thomas Wenski ametoa maelezo juu waraka wa Kanisa, ambao umetoa mchango wa mafundisho ya kijamii ya Kanisa kuhusu heshima ya kazi. Maelezo yake yamelenga katika msisitizo unaotolewa na Papa Francisco, mara nyingi katika hotuba zake kuhusu haki kwa kazi, na hasa heshima katika utu wa mtu.

Marekani, kila tarehe mosi Septemba, huiadhimisha kama Siku ya Kazi, ambayo kwa mara ya kwanza iliofanyika mwaka 1882. Tangu hapo, husherehekewa vyama mbalimbali vya wafanyakazi, kwa ajili ya uimarishaji wa uwezo wa uchumi kwa taifa la Marekani.

Askofu Mkuu Wenski wa Miami, Mwenyekiti wa Tume ya Baraza la Maaskofu Marekani kwa ajili ya Haki na Maendeleo ya Binadamu, ambayo pia hutoa mwanga juu ya hali halisi mbalimbali ya wafanyakazi Marekani, amezungumzia ukosefu wa ajira na matumaini kwa mamilioni ya watu na matatizo yanayo hitajika kupata ufumbuzi.

Askofu Mkuu Francisko, katika tafakari yake, kwa tukio hili la mwaka huu, amewakumbuka Wataktifu Yohane XXII na Yohane Paulo 11 waliotangazwa kuwa Wataktifu na Papa Francis mwaka huu. Amewataja wote wawili kwamba michango yao ilikuwa mikubwa katika mafundisho ya kijamii ya Kanisa juu ya heshima ya kazi na umuhimu wake katika ustawi wa binadamu. Amesema, Mtakatifu Yohane Paulo II, aliitaja kazi kuwa kipengere muhimu katika suala zima la maisha ya kijamii" (Laborem Exercens, No 3) na Mtakatifu Yohane XXIII, alisisitiza haki za wafanyakazi kwamba kila mfanyakazi anapaswa kupata ujira wa haki(Pacem in Terris, No 20).

Aidha amerejea msisitizo wa Papa Francsiko ambaye ameongeza katika maelezo ya watangulizi wake kwamba, kila kazi lazima iandamane na heshima msingi ya utu mtu, sote tukiwa na hali sawa kama watoto wa Mungu. Na alisisitiza umuhimu wake katika kudumisha umoja na mshikamano si tu ndani ya familia lakini pia kijamii na katika ukuaji wa taifa moja.Kazi inatusaidia kutambua ubinadamu wetu na ni muhimu kwa ustawi binadamu. Kazi si adhabu kwa ajili ya dhambi lakini ni njia ambayo sisi, tunapaswa kuifanya kama zawadi kwetu wenyewe na kwa kila mmoja na jamii zetu. Hakuna anayeweza kuendeleza ustawi wake au ustawi wa jamii au taifa bila kazi na heshima na majitoleo ya nguvu katika mshikamano wa watu wote.

Kwa hiyo Askofu Mkuu Wenski, amesema, adhimisho la Siku hii ya Kazi, hutoa nafasi ya kuona jinsi kazi katika taifa la Marekani, inavyokwenda sambamba na maadili ya kujivunia ya utamaduni ma mafundisho Katoliki. Mwaka huu, baadhi ya Wamarekani wamepata ahueni iliyowapa mpumuo wa utulivu na usalama kwa uwepo wa msaada kama kinga dhdi ya ugumu wa maisha. Na myumbo wa ukuaji wa uchumi, unaosababisha pia myumbo katika upatikanaji wa ajira, unatoa himizo kwa taifa la Marekani kujenga ajira zinaonyesha kwamba nchi inaweza hatimaye kuwa na uchumi ponyaji baada ya miaka ya mateso na maumivu ya kimaisha.
Askofu Mkuu Wenski, amesisitiza uelimishaji juu ya maana na heshima kazi , hasa kwa vijana kwa ajili ya kuwajengea matumaini katika kuunda familia zao zilizo bora na imara. Kazi na maisha ya familia huenda sambamba, katika maana kwamba hutegemeana moja kwa jingine. Na hivyo kazi linakuwa ni sharti kwa ajili ya uanzisha familia mpya, kwa kuwa familia inahitaji njia ya kujikimu,kwa njia ya kazi" (Laborem Exercens, No. 10). Na ameshauri kufuata mwongozo wa Papa Franciko, katika kukataa uchumi wa kutengana ila kazi iwe ni utamaduni halisi ya kukutana na kuunda umoja na mshikamano .
All the contents on this site are copyrighted ©.