Kanisa ni mama mwenye kuonea fahari watoto wake. Hili limeelezwa na Papa mapema Jumatano,
wakati akitoa katekesi yake kwa mahujaji na wageni walio fika kumsikiliza katika uwanja
wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican. Katika Katekesi hiyo Papa pia kwa namna
ya pekee, aliwakumbuka Wakristo wanaoteseka, hasa huko Iraq nakuwakumbusha kwamba,
Kanisa kwa maombezi ya Bikira Maria Mama wa Kanisa, daima huwatetea watoto wake ,
na kuteseka pamoja nao katika dhiki zao zote.
Baba Mtakatifu Francisco katika
Katekesi hii kwa mahujaji na wageni, aliendelea kutafakari juu ya Imani ya Mkristo
kama alivyosiistiza kwa mara kadhaa kwamba, haiwezekani kuwa Mkristo wa kweli kwa
kujitenga mbali na wengine, au kwa kutumia nguvu binafsi za kibidamu na ukristo hautengenezwi
katika maabara , lakini kwa yale yanayotokana na matendo mema na kukua katika imani
inayowaunganisha waumini wote katika mwili mmoja ambalo ni Kanisa. Kwa maana hii,
Kanisa linakuwa kweli mama, mama yetu Kanisa. Papa alisisitiza akisema , tazama tu
hata inavyo pendeza kutamka, Kanisa ni mama yetu, ndiye anayetupatia uhai katika
Kristo na hutufanya kuishi kama ndugu katika umoja wa Roho Mtakatifu.
Papa
alitoa mada yake chini ya vipengere 3. Kwanza alilizungumzia umama wa Kanisa, kwa
mfano wa Bikira Maria, mfano ulio bora kuliko mifano yote inayoweza kutolewa, akiangalisha
katika maelezo yaliyotolewa na Wakristo wa mwanzo na pia kwa mwanga wa Mtaguso Mkuu
wa Pili a Vatican (cf. Const. Lumen Gentium, 63-64).Umama wa Maria ukionekana kuwa
hakika ni wa kipekee, uliokamilishwa na utimilifu wa wakati, wakati Bikira alipojifungua
Mwana wa Mungu, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Papa aliendelea kueleza juu ya mwendeleza
wa uhusiano huu wa Mama Bikira Maria na Kuzaliwa kwa Kanisa alilolibeba tumboni mwake,
akisema kweli ulikuwa ni mwanzo wa kuzaliwa upya kwa kila Mkristo katika tumbo la
Kanisa, Kristo akiwa uzao wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi (Rum 8:29) na ndugu yetu
wa kwanza, Yesu aliyezaliwa Maria ni mfano wa kuigwa, na sisi wote tulio zaliwa ndani
ya kanisa. Tunahitaji kuelewa juu ya uhusiano unaunganisha Maria na Kanisa kwamba
, daima hutupa sura nzuri na saburi zaidi katika kulitumainia kanisa, na katika kutambua
sifa za uakatifu wa Mama Maria.
Papa alieleza huku akishangiliwa na waliokuwa
wakisikiliza kwamba, Sisi Wakristo, si watoto yatima, tuna mama, hili ni neema kubwa.
Alisisitiza mara kwamba kwamba, ndani ya Kanisa Wakristo si yatima, kwa kuwa Kanisa
ni mama, Maria ni mama.
Pili, Papa alisema, Kanisa ni letu kwa kuwa tumezaliwa
ndani yake kwa ubatizo. Na hivyo kila mbatizwa , anakuwa ni mwana wa kanisa , na huingia
ndani ya tumbo la kanisa. Na hili linatufanya sisi kukua katika imani na inatuonyesha
sisi, kwa uwezo wa Neno la Mungu, njia ya wokovu kwamba tunaweza kujilinda dhidi
ya kutenda maovu.
Na tatu , Papa alizungumzia juu ya upendo wa Kanisa , akisema
ndani ya kanisa sote tunapendwa kama wana wa mama mmoja, mama ambaye anajali ustawi
wa watoto wake hata akiwa tayari kuyatoa maisha yake kwa ajili yao. Papa amekumbusha
kwamba kanisa si Maaskofu, au Mapadre au watawa peke yao. Kanisa ni jumuiya nzima
ya waamini wabatizwa, kila kubatizwa, mwanaume na mwanamke, na kila lika, vina na
watoto pamoja huunda Kanisa.
Papa alikamilisha kwa kuhoji lakini ni mara ngapi
katika maisha yetu kama wabatizwa, hatuwezi kumshuhudia mama huyu mkuu Kanisa. Tunahitaji
kusali ili kupata ujasiri wa kufanya hivyo. Yesu, anasema, roho wa mama huyu yumo
katika usharika , umoja na uwezo wa kujali mahitaji ya wengine , kusamehe, kufariji
katika kusimama imara katika matumaini.
Na hivyo tujiweka chini ya Mama Yetu
Maria, Mama wa ndugu yetu mzao wake wa kwanza, mwenye kutufundisha kwamba kuipokea
roho yake ya kimama ni katika kukutana na ndugu zetu, katika ukweli wa kupokea, kusamehe
na majitoleo kwa ajili ya wengine katika uaminifu wa kina na matumaini.
Baada
ya Katekesi hii Papa alisalimia makundi mabalimbali ya kijamii, wakiwemo wagonjwa,
wanandoa na vijana. Na mwisho kwao wote aliwapa baraka zake za Kipapa.