2014-09-03 15:33:53

Habari mbalimbali kwa kifupi


Ghasia za Ukraina
Bado kuna wasiwasi mkubwa unaondelea nchini Ukraina kwa sababu ya mapigano katika maeneo ya mashariki ya mji mkuu Kiev.
Waziri wa ulinzi wa Ukraina Bwana Valeri Gheletei aliandika kuwa nchini Ukraina imeingia vita kubwa ambavyo havijawahi kuonekana Ulaya, ambavyo tayari imesababisha makumi na maelfu ya watu kupoteza maisha..
Wanajeshi wa Ukraina waameacha uwanja wa ndege wa Lugansk chini ya ulinzi waasi wa Kirusi.
Ni vigumu kuhesabu waliokufa kutoka Kiev, inadaiwa wanajeshi saba kufariki na wengine 25 majeruhi, katika muda wa saa 24, wanajeshi 260 wametekwa na kufungwa kama wafungwa wa kivita baada ya mapigano makari katika mikoa ya Donetsk.
Pamoja na hali hii inayoendelea kumefanyika mkutano kati wa wawakilishi kutoka Urusi, Ukraina , Osce na kutoka katika kikundi la waasi ambao walitengana na Urusi wakidai kutambuliwa hali zao kwa namna ya pekee kwenye mikoa ya mashariki ya Ukraina. Na mkutano mwingine wa unategemewa kufanyika 5 Septemba 2014.
Pamoja na hayo yote bado kuna utata katika kupata ufumbuzi wa tatizo la nchi hizo mbili kwa na hivyo kutia wasiwasi mkubwa Muungano wa nchi za ulaya ambao bado unatafuta suluhu.
Hayo yalielezwa na Bwana Donald Tusk huko Danzica, Mwenyekiti wa Ushauri wa nchi za Ulaya katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuanza kwa vita vya pili vya dunia iliyoadhimishwa hivi karibuni. Bwana Donald Tusk alisema kuwa wasiwasi wake ni kwamba ipo hatari ya kurudiwa tena vita vile vilivyotokea Septemba 1939.


ITALIA
Shirika la habari la Ansa limeripoti kwamba katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Ulaya ,lilifanyoka hivi karibun huko mjini BRUXELLES limewateua wajumbe wake wawili Donald Tusk wa Poland, nao ni Mwenyekiti wa kudumu wa Baraza la Ushauri la nchi za Ulaya na Mikutano yake Mikuu , na Waziri wa mambo ya nchi za nje Federica Mogherini wa Italia, kuwa wawakilishi Katika Muungano wa nchi Ulaya katika masuala ya siasa za nje na ulinzi.
Pia suala la Ukraina lilijadiliwa katika Mkutano Mkuu wa Baraza hilo la Ulaya, ambamo Bwana Tusk , alilizungumzia akisema kwamba nia kuu Umoja wa nchi za Ulaya ni kufikia amani , ambayo itatokana na juhudi makini za wale walioandaliwa kufanya hivyo na ya kwamba ana uhakika mkubwa kuwa jinsi ilivyojitokeza kwa kipindi kilichopita , Muungano wa ulaya utatafuta njia za kuweza kufikia muafaka wa pamoja katika lengo hilo la amani Ukraina.
Naye Federica Mogherini Mwakilishi wa siasa za nje na ulinzi na Waziri wa nchi za nje nchini Italia aliongezea kusema Ulaya ina changamoto kubwa sana lakini anawashukuru na kuwapongeza viongozi hawa kwa imani kuu waliyo nayo.
Viogozi hawa waliochaguliwa wametanguliza kazi ya kutafuta amani kuwa kipaembele cha juu msingi.
Rais Jamhuri ya Italia Bwana Giorgio Napolitano alimpongeza waziri wa nchi za nje Mogherini kwa kuteuliwa kwake, na pia Waziri mkuu wa nchi ya Italia Renzi alimtakia kazi njema aliyokabidhiwa.


Libia: Wizara ya serikali za mitaa Libya yatekwa na wapiganaji
Libya imekumbwa na ghasia tangu kuagushwa mamlakani ya hayati kanali Muammar Gaddafi aliyepinduliwa na wanajeshi wa Nato wakisaidiwa na wapiganaji wa kiisilamu mwaka 2011.
Taarifa zilizotoka katika serikali hiyo zinasema kuwa ,Watu waliokuwa wamejihami waliwazuia wafanyakazi kuingia katika ofisi za wizara hiyo. Na pia Jumapili 31.08.2014, wapiganaji hao waliteka makao ya ubalozi wa Marekani, hawa ni wakipiganaji miongoni mwao wenyewe wanao tafuta mamlaka.
Maafisa wakuu wa serikali na wabunge walihamia katika mji wa Tobruk, Mashariki mwa nchi hiyo mwezi uliopita. Marekani na mataifa mengine yalilazimika kuwaondoa wafanyakazi wao kutoka nchini humo mwezi Julai huku mapigano yakizidi kuwa makali mjini Tripoli.
Taarifa zinaendelea kueleza kuwa Waziri mkuu Abdullah al-Thinni na baraza lake la mawaziri, walijiuzulu wiki iliyopita ili bunge liweze kuteua serikali mpya.
Nchini Libia viongozi wa hawamu hiyo walikuwa niwa uchaguzi wa pili tangu kanali Gaddafi kuuawa katika mapinduzi yaliyotokea ya mwaka 2011.
Kutokana na ghasia zinazoendelea huko Libya , hata Shirika la habari la Fides limemkariri Balozi wa Papa Martinelli nchini Libia mji Mkuu Tripol akisema kuwa hali sasa inaendelea kuwa shwali , kuna utulivu kidogo kwani mabomu yametulia kulinganisha na siku zilizopita. Ni matumaini yake kuwa neema ya Mungu inaweza kusadia hali iweze kuendelea hivyo kwa utulivu
Balozi anasema kwamba hadi sasa wamepata matatizo makubwa na hasa jumuiya ya wakristo,.
Watu hawa hata kama ni wachache wanakwenda kanisa kwasababu ni furaha ya kukutana.
Mon Martinelli anaongeza kuwa, tarehe 5Septemba ni sikuu ya Mama Teresia wa Kalkuti, wanategemea watafika watu katika sikukuu hiyo. Anamalizia kusema kuwa watu waendelee kuiombea nchi ya Libia hili iweze kupata amani.

AFRIKA YA KUSINI:RAIS JACOB ZUMA AFANYA MKUTANO WA DHARURA N
Jumamosi Sept 30 Jeshi lilizingira makao ya waziri mkuu na kumlazimu kukimbilia nchini Afrika Kusini pamoja na mawaziri wake. Inaarifiwa kuwa jeshi lilikuwa linamzuia waziri mkuu kumfuta kazi mkuu wa majeshi.
Hata hivyo jeshi limekanusha madai hayo likisema lilipokea taarifa kuwa polisi walikuwa wanapanga kuhami vikundi vya vijana ambao wangefanya maandamano kulazimisha waziri mkuu kufungua vikao vya bunge. Maandamano hayo hayo lakini yalisitishwa.
Wakati huo Serikali ya Afrika Kusini ambako waziri mkuu huyo amepata hifadhi, imesema haitastahamili mapinduzi kufanyika katika nchi hiyo.
Inaonekana kulikuwa na njama ya mapinduzi nchini humo, lakini jeshi linasema kila kitu kiko shwari. Baadhi ya viongozi wa kanda hiyo,wamefanya mkutano kujadili hatua watakazochukua, ambapo Jumapili usiku ulifanyika mkutano huo wa dharura kati ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na waziri mkuu wa Lesotho, Thomas Thabane,
Mkutano huo ulilenga kutafuta nyenzo za kumaliza mgogoro wa kisiasa katika ufalme huo mdogo.Mawaziri wa ulinzi na mambo ya nje wa Namibia na Zimbabwe walishiriki kwenye mkutano huo ingawa taarifa zaidi zilizojadiliwa kwenye mkutano huo bado hazijatolwa.


UZINDUZI MPYA WA KUKATA TIKETI TANZANIA
Meneja Mkuu wa Travelport, Eliasaph Mathew ameishauri Serikali ya Tanzania kupunguza kodi katika huduma za usafiri wa anga ili watanzania wengi wamudu kuutumia usafiri huo katika shughuli zao za kiuchumi.
Ushauri huo umetolewa Mosi September wakati wa uzinduzi wa mtandao mpya wa ukataji wa tiketi za ndege uitwao (PreciseSky), utakaosaidia mashirika madogo ya ndege kuhimili ushindani wa biashara ya usafiri wa anga.
Trevelport ni kampuni ya kimataifa inayojihusisha na kuyapatia mashirika ya ndege duniani mifumo ya ukataji wa tiketi.
Meneja huyo alisema kuwa “Hii inadidimiza uchumi kwa sababu mtalii anaona heri aende Uganda au Kenya anakotozwa kidogo wakati Tanzania ndiyo mojawapo ya vivutio vingi zaidi vya utalii kulinganisha na nchi za Afrika Mashariki, sasa hivi tena wanapendekeza VAT iwekwe kwenye usafiri wa anga”.
Aliongeza “… Nayo hiyo itadhohofisha biashara katika usafiri wa anga maana hakuna nchi yeyote duniani inayotoza VAT sekta ya usafiri wa anga,”
Aliendelea keleza kuwa hivi sasa watumiaji wa usafiri wa anga duniani wanapata mahitaji yao kupitia mitandao ikiwemo ununuzi wa tiketi, sehemu ya kukaa kwenye ndege, chakula na hoteli wanazotaka kufikia kwenye nchi wanazokwenda hivyo kuna haja kwa makampuni yanayotoa huduma kwenye sekta hiyo kwenda na wakati.
Pia Meneja wa mtandao huo mpya wa Precise Sky, Gloria Urasa alisema mfumo huo ni mpya Tanzania na utayasaidia mashirika madogo ya ndege hapa nchini kuonekana duniani kwa kuongeza sehemu za kuuzia tiketi za ndege zao hivyo kuzidi kukua kibiashara.
All the contents on this site are copyrighted ©.