2014-09-02 10:24:06

Mechi ya wachezaji maarufu kwa ajili ya amani duniani.


Papa kwa wachezaji wa madhehebu soka: dini na michezo wanaweza kushirikiana kwa amani
(Vatican Radio) Mechi ya soka kwa ajili ya amani ilifanyika Jumatatu usiku kama yalivyokuwa matamanio ya Papa Francisko. Timu za wachezaji ziliundwa na wachezaji 50, ambao ulikuwa ni mchanganyiko wa wachezaji mashuhuri wa zamani na mabingwa wa sasa,Mechi hiyo ilifanyika katika uwanja wa michezo wa Olympic hapa mjini Roma

Baba Mtakatifu Francisco, nyakati za jioni alikutana na baadhi ya wachezaji mashuhuri walioshiriki katika mechi hii. Papa alizungumzia tukio hili akisema, ni ishara nzuri yenye kuonyesha kwamba, inawezekana kujenga utamaduni wa kukutana na dunia ya amani, ambapo waumini wa dini mbalimbali, wanaendelea kuhifadhi utambulisho wao wa kidini, na kuishi pamoja kwa amani na kuheshimiana. Papa alitoa shukrani zake za dhati hasa kwa watu na mashirika ambayo yamechangia utambuzi wa tukio hili. Hasa Taasisi ya "Scholas occurrentes," ambalo ni tawi la utendaji wa kazi katika Taasisi ya Kipapa Taaluma ya Sayansi, na pia kitengo cha "Pupi Foundation Onlus".

Katika hotuba yake, alikemea tabia ya “ubaguzi” akisema ni sawa na "dharau", na dharau ni sumu kali katika maisha ya umoja na mshikamano. Na alitoa wito kwa dunia kuachana na tabia hii mbovu, badala yake watu wote wapendane na kujenga mshikamano na umoja, kama inavyokuwa kwa timu za wachezaji, hucheza pamoja bila ubaguzi wowote.

"Dini," aliongeza, ni gari la amani la maisha na kamwe si gari la chuki. " Dini na mchezo, "ni alama wazi katika ushirikiano na umoja, ingawa huwa ni pande mbili zinazopigana hufanikisha tukio katika hali ya amani , umoja na kuburudisha, na hivyo linakuwa ni somo zuri kwa jamii, kuona kwamba kumbe inawezekana kuishi kwa amani katika hali zetu mchanganyiko wa utamaduni, imani na elimu. Alionya, kwa jamii ya leo, ambayo kwa ujumla imestraabika, kumwinulia mwingine panga, limekwisha kuwa jambo la zamani lililopitwa na wakati. Leo hii Silaha inayofaa kuliko zote pale panapotokea mtafaruko wa kutoelewana katika baadhi ya vipengere vya maisha ni majadiliano. Ni kuketi pamoja kwa amani, kuelimishana na kutoa jibu linalofaa kwa manufaa ya wote. Kumkata mwingine panga hakuondoi tatizo bali hujenga matatizo zaidi. Kwa hiyo kama ilivyo timu za wachezaji ni kucheza pmoja katika majadiliano hadi mshindi anapatikana kwa amani.
Papa Francisco aliongeza, katika mechi ya leo usiku, ambayo inachezwa katika hali isiyo ya kawaida, ni tukio muhimu, ambalo linataka kutoa ujumbe kwa wote kwamba, kama ilivyo muhimu kwa wachezaji kupiga mbio za kukimbizana na mpira wa miguu, ni muhimu pia kukimbizana na maisha kama ndugu, ni kupanua moyo wa kumpokea mwingine kama ndugu katika ya furaha na fadhila. Hii ni moja ya siri za maisha. Unapopata mpira si kubaki nao muda wote lakini unampasia mwingine. Ndivyo maisha yanavyopaswa kuwa. Using’ang’anie vile unavyovipata lakini mpasie pia mwingine kwa furaha na amani. Asanteni sana, Papa alikamilisha hotuba yake fupi kwa wachezaji mashuhuri.
Na kwa ajili ya kuendeleza moyo huu wa ushirikiano katika michezo , Ofisi ya Baraza la Kipapa kwa ajili ya utamaduni, kwa kushirikiana na wabia wengine linaendesha semina ya siku tatu, inayohudhuriwa na wawakilishi kutoka vyama vya michezo Katoliki vya Marekani, Uingereza, Italia, Mexizo, Slovakia na Malta. Pamoja na mengine yatakayogusiwa piani pamoja na Mkutano Mkuu wa Dunia wa Michezo na Amani , utakaofanyika mjini Vatican Septemba 2015.
All the contents on this site are copyrighted ©.