2014-09-01 15:40:12

Semina ya kimataifa juu ya Michezo kwa ajili ya binadamu


Tarehe 1Sept 2014 katika uwanja wa michezo Olympio wa Roma kutafanyika kandanda ya michezo kati ya muungano wa madhehebu mbalimbali ya dunia.

Kutokana na fursa hiyo ya michezo itakayo fanyika Baraza la ushauri na utamaduni la kipapa kwa ushirikiano , na Ofisi ya taifa ya kichungaji ya muda uria , Ofisi ya michezo na utalii ya Baraza la Maaskofu Italia, Shirika Yohane Paulo wa Pili kwaajili ya michezo, watakutana na wahusika wa Taasisi za Kimataifa katoliki za michezo kuwa na siku ya majadiliano, na kaulimbiu “mchezo ni kwaajili ya binadamu”, <>
Ni semina ya siku tatu itakayo fanyika katika Ofisi ya Baraza la mashauri na utamaduni la kipapa mjini Vatican, na watakao udhuria ni pamoja na wawakilishi kutoka vyama vya michezo vya kikatoliki vya Marekani, Uingereza, Italia, Mexico, Slovakia, na Malta

Pamoja na mengi yatakayogusiwa katika mkutano huo ni pamoja na kuandaa mkutano mkuu wa dunia utakao kuwa na kaulimbiu juu ya “ Vatican Mkutano wa kimataifa wa Michezo na Imani Septemba 2015 (Vatican Global Conference on Sport and Faith) Sept 2015.
Mkutano huo utakuwa wa kihistoria kufanyika kwa mara ya kwanza Makao Makuu ya kharifa wa mtume Petro hapa mjini Roma kati ya viongozi wakuu wa Kimataifa , viongozi wote wa michezo, duniani na viongozi wa dini kwaajili ya kujadili changamoto zinazokabili michezo duniani.
Ndugu wapendwa wasikilizaji wa Radio vatican , pamoja na kauli mbiu ya semina hii ya “ Mchezo ni kwaajili ya binadamu” kuanzia matokeo ya utamaduni kufikia kukutana na tamaduni, utakaofanyika 1Septemba 2014;
Je tunaweza kukumbuka kitu gani kuhusu michezo katika jamii zetu na katika tamaduni zetu?
Je leo hii michezo ni kwaajili ya binadamu kweli au inavuka mipaka ya ubinadamu?
Ni makala yetu leo ninayotaka tupate kujadiliana kwa pamoja.
Kwanza kabisa katika ujumbe wa video kwenye ufunguzi wa kugombea kombe la dunia la mwaka huu 2014 huko nchini Brazil Papa Francis alisema mambo muhimu juu ya michezo pamoja na hayo alitoa kauli kuwa michezo “ni chombo cha kuwasilisha tunu msingi katika kuboresha ubinadamu na katika ujengani wa jamii ya amani na ya kindugu”
Kwa kauli hiyo yatari tunapata wazo kuu juu ya michezo kwa ujumla ya kwamba michezo imekuwa na lengo kuu msingi tangu zamani za kale la kujenga undugu na amani.

Kama mchezo ni chombo cha kuwasilisha tunu ya binadamu mwenyewe, kujieleza mwenyewe, kukubalika mwenyewe na kujikubali, inamaana kwamba nchi yoyote haiwezakani kutambulikana na utaifa wake bila kuwa na utamaduni wao, na mojawapo ya viungo vya tamaduni hiyo vinavyounganisha katika duniani hii ni “michezo”.
Mfano kuna baadhi ya mataifa mbali ambayo wameweza kujitambulisha kwa mavazi, na ishala mbalimbali … ukiona “vazi “ fulani tayari unajua ni kutoka nchi gani…au ishala fulani kama vile sisi afrika mashariki “wamasai”, tayari unajua wanatokea wapi, hivyo basi michezo ni chommbo muhimu sana katika kuendeleza jamiii. Aidha michezo uweza kuwa kielelezo kikubwa na utambulisho wa taifa katika kutoa burudani, kujenga nidhamu , kujitangaza kiuwezo na kukomaza afya, ya mwili na akili .
Mara ngapi nchi moja na nyingine inajitangaza vipaji vya wachezaji wake inaposhiriki michezo ya kitaifa na kimataifa (mifanotunayo mingi, sasa hivi tunasikia ni jinsi gani wachezaji wa mipira watahama kutoka timu moja hadi nyingine mara baada ya kombe la dunia , maana sasa hivi wako katika soko...)

Kutokana na umuhimu wa michezo katika jamii kila kipindi cha kihistoria, binadamu amekuwa akishiriki michezo katika tamaduni mila na sanaa,tunajua michezo ya mila na desturi tangu zamani , imekuwepo, mieleka, kuruka, kukimbia kulenga shaba ya mishale , kuogelea nk.
Ni michezo iliyokuwa inalenga kujiamini na kuwa na utambulisho wa kila jamii ambayo iliitwa ya jadi, hata ndugu zetu waliopelekwa kwenye utumwa na kukutana na watu wa mataifa mbalimbali walieneza jadi zao katika michezo hiyo, iliyowasaidia sana kukabiliana na matatizo yaliyokuwa yanawakumba katika utumwa huo.
Lakini ndugu wasikilizaji wapendwa baada ya michezo ya kisasa kuingia kama mipira ya miguu, mipira ya meza, ndondi, mbio, baiskeli,magari ya mashindano, mashindano ya farasi na michezo mingine mingi historia ya jadi ikalegeza thamani yake, na kuanza kutawaliwa kwanza fedha na ushindani
Hatuwezi kusahau kwamba michezo ya jadi kwanza ilikuwa inalenga undugu zaidi , urafiki zaidi burudani zaidi ,katika kushirikiana kwa pamoja na kuishi kwa amani.
Leo hii katika viwanja mbalimbali vya mipira, kuna uwoga wa kurudi salama au kutokurudi salama, ni hatari kubwa.
Millenia ya leo inazo changamoto nyingi ambazo zimejitokeza kwenye michezo kama vile, kinachotangulia ni fedha, na ushindani, au kuwepo na madharau ya rangi za watu, kutaka kushinda kwa kila njia, wakati mwingine hata watu wanaofanya michezo hiyo kupenda kutumia hata madawa ya kujiharibu mwili hili wawe na guvu za kushinda.

Ndugu wasikilizaji wa radio vatican, changamoto ni nyingi kwani mabadiliko ya jamii yetu wazazi wengi kutowafundisha watoto umuhimu wa michezo ni nini, kwasabau watoto walio wengi ukisema mchezo kitu cha kwanza kichwani ni kufikiria kushinda kabla ya burudani na furaha ya kushiriki na wengine, na ndiyo maana utakuta watoto wengine hawapendi kushiriki michezo kama ngoma muziki akisema mimi siwezi maana mwenzangu ndiyo aliye na uwezo.

watoto walio wengi wanapokwenda kwenye michezo tayari wana wazo lazima washinde tu, na kumbe uwajibikaji wa jamii zetu kuanzia katika familia muhimu sana kuwafundisha tangu utoto umuhimu wa miichezo ya pamoja kwanza ni kufurahi , kunyosha viuongo kwa ajili ya kutunza afya bora na siyo tu kushinda na kupokea zawadi.
Maana katika mchezo lazima mmoja tu ashinde, mfano wa hivi karibuni tumeona machozi , masikitiko na majonzi kwenye kombe la dunia.

Katika barua ya kwanza Mtakatifu Paulo kwa wakorinto alijua wazi ushindani huo wa michezo ambao unaweza kutufanya tusahau misingi na thamani kubwa ya binadamu, yaani mimi na mwenzangu na Mungu.

Alisema“ Je hamjuhi ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio , hupiga mbio wote , lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo ili mpate. Na kila ashindaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao ufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo: bali sisi tupokee taji isiyoharibika” (1Wakor 9,24-26)

Na kumbe michezo ina utajiri mkubwa kwa binadamu si katika bihashara au malumbano, bali utajiri wa kuunganisha watu, kabila , jamii, taifa na mataifa nikitoa mfano wa changamoto za zinazokabili nchi za Ulaya ,ukimbizi na uhamiaji kupitia njia ya baharini , siku hizi tumeona watu wengi na hasa vijana waliopokelewa katika vituo mbalimbali hapa nchini Italia hata kama hawajuhi lugha ya mahalia , lakini kinachowaunganisha , ni zile talanta zao walizo nazo za kucheza michezo mbalimbali, na ndiyo maana ya semina ambayo itafanyika kwaajili ya kuandaa mkutano mkuu wa mwaka kesho 2015
Michezo izidi kuoboreshwa katika tamaduni zetu, hili iweze kutuunganisha,badala ya kututenganishe, iboreshe utu kwanza kuliko kujali mali , ndipo tutajenga jamii ya utu kweli na yenye kupendana kama ndugu.All the contents on this site are copyrighted ©.