2014-09-01 12:44:48

Masista, waamua kukabiliana na matatizo kwa karama zaoChama kinacho unganisha watawa wa kike (Masista ) katika mkoa wa Afrika Mashariki na Kati (ACWECA) kimehitimisha Mkutano Mkuu wake wa wiki mbili, uliofanyika Lusaka, Zambia, kwa kutoa tamko lake jipya lililotiwa saini na Mwenyekti Mpya wa ACWECA, Sista Prisca Matenga, ambaye ni Pia ni Mama Mkuu wa Shirika la Mabinti wa mkombozi (DOR).

Mkutano huu pia ulichagua wajumbe wapya wa Bodi Tendaji ya ACWECA, ambao ni Sr. Prisca Matenga wa Zambia kama Mwenyekiti mpya. Wengine ni pamoja na Sr. Ann Henrietta Nyangoma (Makamu wa Chairperson- Kenya), Sr. Susan Ndezo (mjumbe, Uganda), Sr. Clementina Nkandira (mjumbe, Malawi), Sr. Therese Nyoni (mjumbe Zambia), Sr. Sr. Lucy Maliekal (mjumbe Tanzania), Sr. Mary Daniel abut (mjumbe S. Sudan), Sr. Noha Mykadi Koko Angilo (mjumbe Jamhuri ya Sudan). Wengine ambao wamechaguliwa Wawakilishi ni kutoka Eritrea na Ethiopia.

Katibu Mkuu wa ACWECA ni Sr Enelesi Chimbali wa Shirika la Watumishi wa Bikira Maria (SBVM), ambaye pia ni mjumbe kutoka Chama kinachowaunganisha Masista nchini Malawi (AWRIM).

Tamko kutoka Mkutano huu Mkuu wa 16 wa ACWECA, ulioongozwa na Mada mbiu: “Nenda, usiongope kutumikia"limeanza na salaam kwa waamini wote wa Kanisa Katoliki na watu wote wenye mapenzi mema!

Na kwamba, Chama cha Wanawake walioyaweka maisha yao Wakfu wa Afrika Mashariki na Kati (ACWECA) kina wasiwasi na hali ya kisiasa ilivyo katika baadhi ya maeneo ya mkoa wao yaani, Eritrea, Ethiopia, Sudan Kusini, na Jamhuri ya Sudan. Wao kama Wanawake Katoliki walioweka maisha yao wakfu wa kumtumikia Mungu, wakiwa katika Mkutano Mkuu uliofanyika katika Hotel ya Andrews Motel, Lusaka, Zambia, Agosti 16-29, 2014, wameweza kujumuiya pamoja kaika Ibada tolea sala zao kwa pamoja na kuwa na muda wa kujadili mazingira ya nyakati hizi, wakiongozwa na kaulimbiu; Nenda , usiogope na tumikia, katika mtazamo wa kujenga majitolea ya sadaka ya Masista wanaofanyakazi kazi na kuhudumia kwa ujasiri katika maeneo hayo.

Na kwamba wamepania kuanza na wao wenyewe kama mtu binafsi ,katika kuiongoza njia ya maisha yaliyosimikwa katika maadili na tunu za Injili na Kanuni za kuheshimiana na kumheshimu kila mtu. Na kwa pamoja wameweza kujadiliana na kushirikishana uzoefu na njia zinazoweza kuboresha ufanisi katika utendaji wa majukumu yao kama Masista.

Katika mwanga wa Kaulimbiu"Nenda, Usihofu na Tumikia, wao kama wanachama ACWECA wameahidi:-Kukumbatia na kukuza tunu za Injili katika haki, amani, maridhiano, matumaini na Mshikamano. -Kuongeza bidii binafsi endelevu katika vyama yote ya kitaifa. -Kukuza, kuongeza, kuzamisha na kuimarisha maisha ya kidini kwa njia ya malezi maisha katika mipango Mitakatifu. -Kuimarisha mitandao na Mikutano nyingine Taifa na Miundo Kanisa. -masuala muhimu ya kichungaji yanaoonekana kuwa ya kidharura zaidi hasa katika utetezi na udumishaji wa haki ya kijamii na maendeleo,-Kuhamasisha kila chama kutoa mafunzo kwa Masista,katika mwelekeo wa kiroho na sheria ya Kanisa.
-Kuandaa mipango yenye kutoa kipaumbele maalum kwa wanachama wanaoishi katika mazingira magumu ya kijamii kwa lengo la kukuza haki za binadamu na heshima kwa binadamu wote (umaskini, biashara ya binadamu ...). -Kuendeleza mazungumzo baina ya dini
Hatimaye, wanaonyesha kutambua na kukiri kwa moyo wa shukurani, kwa ukarimu wa Chama cha Masista na watu wa Zambia, kwa ukarimu wao walio watendea kama wenyeji wa Mkutano huu. Pia tamko la Acweca, limetoa shukrani za dhati kwa wafadhili wote wa ndani na nje ya nchi ambao kwa ukarimu wa mkono wao, mkutano umekuwa wa mafanikio. Na wameomba Baba wa Ukarimu wote awarudishie kwa kuwajaza na wingi wa baraka katika kazi zao na familia zao.
Mungu awabariki watu wa ACWECA. Na wametoa wito wao kwa Papa , “Nenda, usiogope na tumikia,Papa Francisko!
Tamko lilitiwa sahihi na Sista Prisca Matenga, DOR , Mwenyekiti wa ACWECA, Agosti 27, 2014.
All the contents on this site are copyrighted ©.