Wakristo Gaza wauishi wito wa Papa :Kuweni Chumvi na Mwanga wa dunia
Padre Jorge Hernandez, mmishonari wa Taasisi ya Neno Aliyefanyika Mwil, ambaye ni
Paroko katika Parokia ya Gaza, akizungumza na Redio Vatican Radio, Ijumaa iliyopita
alieleza kwamba , Ujumbe wa Papa aliowaachia Wakristo wa Gaza, umekuwa muhimu katika
kuwaunganisha, licha ya kukabiliwa nahali ngumu kama Wakristo wanaoishi katika eneo
hilo. Na tena wakati wa machafuko, hufarijika kwamba, Papa yu karibu nao siku zote.
Padre Hernandez aliiambia Redio Vatican, baada ya kukutana na Papa Francisco,
kukutana aliko kuita neema na baraka kubwa kwake, ingawa haikuwa mara ya kwanza. Katika
mazungumzo yao, Papa Francisco aliendelea kutia moyo Jumuiya ndogo Katoliki ya Gaza,
akiitaka idumu na iendelee kuwa “chumvi ya dunia katika nchi ya Gaza. Na kwamba Yeye
pia amekuwa akiguswa na ujumbe wa ushuhuda unao tolewa na Papa kwa Kristo. Na ndivyo
pia jumuya ya Wakatoliki Gaza,wanauishi wito wa Papa kama wito maalum katika kumshuhudia
Yesu Kristo katika nchi yao, ambayo ni nchi ya Yesu, kama nyumbani, nchi iliyo shuhudia
mateso na kifo na ufufuko wake Kristo.
Gaza ina wakazi wapatao karibia milioni
mbili. Jumuiya ya Wakristo ni ndogo sana, wakiwa jumla 1,300 kati yao Wakatoliki
ni 136. Na uhusiano kati ya Wakristo ni mzuri sana. Padre Hernandez alisema,
uwajibikaji wa Papa Francisko kwa Wakristo wa Gaza, imekuwa ni sementi inayowaimarisha
kiimani na katika kuwafariji, hasa katika kumshuhudia Mkuu wa Amani Yesu Kristo. Na
kwamba, watu wa Gaza wanatumaini, amani iliyopatikana sasa kati ya vikosi vya Israel
na Palestina, itakuwa ya muda mrefu. Watu wote wamechoka na vita, wamechoka na mateso.
Na sasa inaonyesha wengi kupata ufahamu kwamba, hakuna anayeweza kufanikiwa iwapo
kuna vita. Kila upande huathirika kwa njia moja au nyingine. Na hatima yake, hakuna
anayefaidika kutokana na vita, wote hupoteza.
Padre Hernandez anatumaini kwa
baraka za Mungu, wataendelea kuwa na nguvu za kuanza tena maisha mapya. Na ili kujenga
amani ya kudumu, Padre Hernandez alisisitiza ni lazima kujenga amani na haki. "Amani
inahitaji kujitoa sadaka, na inawezekana.
Na alitumia muda huu wa kuzungumza
na Redio Vatican , kutoa shukurani zake kwa watu wote duniani ambao wamekuwa karibu
na jamii yake, hasa katika kipindi cha majaribu katika wiki za hizi karibuni. Muda
ambao umekuwa mugumu na ambamo waliyatolea mateso yao kama sadaka katika kuombea amani
hasa kwa ajili ya wagonjwa. Alibainisha idadi kubwa ya Wakristo katika Parokia yake
ya Gaza, mara nyingi hutolea sala, misa na ibada zingine kwa nia za kuwakumbuka wale
wanaoomba pia kwa ajili yao. “Nataka kuchukua fursa hii," alisema, "kusema asante,
na Mungu akubariki."