2014-08-28 16:11:45

USCCB- miaka 50 ya haki za kiraia Marekani.


Kanisa Katoliki Marekani, linashiriki katika sherehe za Jubilee ya maadhimisho ya miaka 50 ya Kitaifa ya Harakati za haki za Kiraia, kwa kuchapisha mfululizo wa habari zinazo onyesha mafanikio katika kipindi hiki na uhusiano wake na kanisa.
Taarifa inasema, kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 tangu kuanzishwa vikundi vya utetezi wa haki za kiraia Marekani, Tume ya Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani '(USCCB) kwa ajili ya mambo ya Wamarekani wenye Asilia ya Afrika, itatoa makala mfululizo kuonyesha mafanikio ya kipindi hiki cha miaka hamsini na uhusiano wake na Kanisa Katoliki.

Na kwamba katika kipindi kijacho cha miezi 12 ijayo, taarifa za Tume, zitagusia Mapambazuko ya Uhuru Mississippi (Juni-Agosti 1964); Sheria ya Haki za Kiraia (Julai 1964); na Maandamano kutoka Selma hadi Montgomery (Machi 1965); na maadhimisho ya miaka 50 ya Sheria ya Haki za kupiga kura Agosti 2015.

Kipindi hiki cha utetezi wa haki za kiraia ni jambo muhimu katka historia ya Marekani. Na kwa nji amb alimblai za kujenga,Mapadre, Masista , Mabruda na Walei Katoliki , wamehusika katika juhudi hizi za kutetea haki za raia Marekani alisema Askofu Shelton Fabre ya Houma-THIBODAUX, Louisiana, mwenyekiti wa Kamati Ndogo. Na alikumbuka ushiriki wa zamani wa Kanisa Katoliki, katika mapambano hayo muhimu ya kihistoria uliotoa changamoto kwa waamini kuendelea na utendaji huo ambao leo hii mafanikio yake yameonekana kwa watu wa jamii zote na makabila.

Na kwamba makala zitakazokuwa zikitolewa zinalenga kuwa msaada wa kukuza majadiliano na midahalo katika Parokia, mashuleni, vikundi Katoliki na wengine, kuweza kuchunguza jinsi matukio yanavyoweza kusaidia kusafisha njia ya ujenzi wa uhusiano mzuri kati ya tamaduni. Pia mradi wa AIMS, unalenga kuinua 'Mazungumzo baina ya vizazi, juu ya maana ya urithi wa kihistoria na kuangalia katika siku zijazo na kuonyesha ushiriki wa Kanisa Katoliki na viongozi wake, kihistoria na changamoto za nyakati.

Maadhimisho ya Jubilee hii, pia itatoa fursa ya kujadili mafundisho ya Kanisa Katoliki ya kijamii.
Tafakari juu ya Mafundisho ya Kanisa ya Jamii kutoka katika mtazamo wa historia ya haki za kiraia inatoa nafasi ya kuapta ueelwa zaidi na kuwa mwanafunzi aminifu zaidi wa Yesu Kristo,aktika jitihada za kuyaishi mafundisho haya ya kijamii katika nyakati hizi, Askofu Fabre alisema.

Makala hizo zinaweza patikana katika:










All the contents on this site are copyrighted ©.