2014-08-28 16:00:55

Papa akutana na Waziri wa zamani Paulo Bhatti


Jumatano, Baba Mtakatifu Francisko, alikutana na Dr Paul Bhatti, Waziri wa zamani kwa ajili ya Mshikamano wa Kitaifa na makundi madogomadogo ya waumini wa dini mbalimbali Pakistani. Dk Bhatti alikuwa kati ya waliohudhuria Katekesi ya Papa ya Jumatano, akiwa yeye na mama yake, wote wawili ni wakatoliki.

Dr Bhutti ambaye ni ndugu wa Shabhz Bhatti , aliyeuawa kikatili mwaka 2011 na mashabiki wa Uislamu, alipata muda mfupi wa kuzungumza na Papa Franciko. Baba Mtaktifu Francisco katika maongezi yao alionyesha masikitiko yake kwamba Wakristo wengi wanaendelea kuteseka duniani kote kutokana na imani yao. Nae Dr Bhatti na mama yake walitoa mwaliko kwa Papa Francisco , aitembelee jumuiya ndogo Wakristo Pakistani.

Dr Bhutti baada ya kukutana na Papa aliwaambia wanahabari kwamba, kwake imekuwa ni heshima kubwa na muda muhimu na wa kipekee. Na katika mahojiano na Redio Vatican, aliikosoa jumuiya ya kimataifa kwamba, kuna udhaifu katika utendaji wake hasa katika kukomesha mateso na mauaji dhidi ya Wakristo. Na kwamba ni muhimu kutambua mzizi wa ubabe wa kidini na ughaidi na kuupatia dawa ya kukomesha. Aidha alizungumzia ujasiri wa baadhi ya Waislamu wasiokuwa na ubabe wanaotetea Wakristo na kulaani vikali unyanyasaji wa watoto, na hasa utiaji wa kasumba tangu wakiwa na umri wa mdogo kutoogopa kuua.








All the contents on this site are copyrighted ©.