2014-08-27 09:21:53

Wanajeshi wa Nigeria watorokea Cameroon


Wanajeshi 480 wa Nigeria wametorokea maisha yao nchi jirani ya Cameroon kufuatia makabiliano makali dhidi ya wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram.
Msemaji wa jeshi la Cameroon Luteini Kanali Didier Badjek amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa wamepokonywa silaha na sasa wamewekwa katika shule .Mapigano hayo yanaendelea karibu na mji ulioko mpakani wa Gamboru Ngala.Mapigano hayo yanawadia saa chache tu baada ya wapiganaji hao wa Boko Haram kutoa kanda ya video ambayo walitangaza kuundwa kwa himaya ya Kiislamu kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau alizungumza kwenye kanda ya video iliyotolewa ili kupongeza wapiganaji wake kwa kuchukua udhibiti wa mji wa Gwoza mapema mwezi huu.Lakini haijabainishwa iwapo Bwana Shekau ameahidi kutii Muungano wa wapiganaji wa kundi la kiislamu la Islamic State inayotawala sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Iraq na Syria.








All the contents on this site are copyrighted ©.