Baba Mtakatifu Francisko, anatazamia kufanya ziara ya Kichungaji ya siku moja nchini
Albania mwezi ujao Septemba, kwa lengo la kuhamasisha mshikamano na umoja wa kitaifa
kwa nchi hiyo ambayo kwa muda mrefu iliteswa na utawala wa udikteta wa kikomunisti,
uliowatenga pia wananchi wake na nchi zingine duniani.
Albania, nchi ya kuzaliwa
ya Mama Mtakatifu Tereza wa Calcutta, katika miaka ya 1990, makumi ya maelfu ya maskini
wa Albania, walikimbilia Italia, wakivuka Bahari ya Adriatic katika vyombo hafifu
vilivyo hatarisha maisha yao, zikiwemo boti za wavuvi. Watu walikimbia mateso na
dhuluma zilizokuwa zikifanywa na utawala wa wakati huo, wengi wao walipokelewa na
kuingizwa katika maisha ya Italia.
Papa Francisco wakati wa sala ya Malaika
ya Jumapili moja, aliwaambia waamini waliofika kusali katika uwanja wa Kanisa kuu
la Mtakatifu Petro kwamba, ana hamu ya kuitumia ziara yake Septemba 21 Albania, walau
kutoa msaada mdogo kwa jamii Katoliki maskini wa Albania.
Theluthi mbili
ya raia wa Albania wapatao milioni 3.2 ni Waislamu ambao huishi kwa amani na kundi
dogo Orthodox, Katoliki. wakati wote wa utawala wa kidikteta wa kikomunisti kati ya
mwaka 1967-1990, hawakuwa na utendaji wowote wa kidini katika maisha ya kijamii.
Waziri
Mkuu Kialbeni Edi Rama amesema ziara ya Papa Itasaidia kukuza maadili hasa kujenga
ushirikiano na amani miongoni mwa watu wa imani na makabila mbalimbali . Hii itakuwa
ni mara ya pili kwa Albania kutembelewa na Papa, mara ya kwanza lilitembelewa na Papa
Yohane Paulo II, baada ya kuangushwa kwa utawala wa kikomunisti mwaka 1993. Nchi
ya Albania ina ukubwa wa eneo km ² 28,748 ,Idadi ya Watu milioni 3.250, ambao kati
yao Wakatoliki ni 517,000 wanaohudumiwa na Majimbo 6 yanayundwa na Parokia 124 na
vigango 25 . Kuna Maaskofu 8 , Mapadre wa Jimbo 54, Mapadre Watawa 93 , Mashemasi
wa kudumu 2 , Mabruda 16, Masista 478, Wamisionari walei 36 na Makateksta 331. Kuna
shule za msingi 54, sekondari sekondari 14 – taasisi za masomo ya juu na vyuo vikuu
5. Hospitali 8, Zahanati za upasuaji 29 na nyumba kwa ajili ya wazee au walemavu
16, Yatima 16 .