Josef Wesolowski hana tena hadhi ya Kidipolomasia Vatican
Mkurugenzi wa Ofisi ya Habari katika Jimbo la Papa , Padre Federico Lombardi, SJ,
siku ya Jumatatu alithibitisha kuwa, Mjumbe wa Kitume wa zamani, Josef Wesolowski,
ni kweli amekata rufaa dhidi ya hukumu ya kumvuliwa hadhi ya Kidiplomasia na kuwa
mtu wa kawaida mlei. Vatican imemvua hadhi ya kidiplomasia kutokana na tuhuma zilizotolewa
dhidi yake kuhusu unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto, akiwa mwakilishi wa Papa
katika Jamhuri ya Dominika, tuhuma zilizo tolewa Agosti mwaka jana. . Na kwamba rufaa
yake itasikilizwa na kutolea maamuzi wiki chache zijazo, pengine mwezi Oktoba 2014.
Padre Lombardi alifafanua mbele ya waandishi wa habari kwamba, mwakilishi
huyo wa zamani wa Jimbo la Papa, katika kisiwa cha Jamhuri ya Dominika, alivuliwa
cheo hicho mara baada ya tuhuma kutolewa dhidi yake , na hukumu kutolewa mapema mwaka
huu kwa mujibu wa sheria za Kanisa. Na mara baada ya mchakato wa rufaa yake kukamilika,
Wesolowski anaweza kupambana na mashtaka ya makosa ya jinai katika mfumo wa mahakama
za kawaida.
Padre Lombardi aliendelea kuweka bayana kwamba , ni muhimu
kutambua kwamba, Nuncio wa zamani Wesolowski kwa sasa hahusiki na kazi zozote za
kidiplomasia kwa Jimbo Takatifu, na hiyo ina maana kuwa hana tena kinga ya kidiplomasia,
aliyokuwa nayo awali. Na utaratibu wa idara ya mahakama ya Vatican katika kezi kama
hii , itaendelea kusikilizwa mara uchunguzi utakapokamilika na hukumu itatolewa kisheria.
Padre Lombardi alieleza hili akirejea maelezo potofu ambayo yamekuwa yakitolewa
katika baadhi ya vyombo vya habari, siku chache zilizopita. Alionyesha mshangao juu
ya upotoshwaji huo, akisema, ni muhimu kutambua kwamba, tangu mwanzo wa kesi, mamlaka
ya vatican, ilitoa maelezo sahihi juu ya jambo hili, tena bila kuchelewa katika
mwanga wa ukweli kwamba Nuncio wa zamani Wesolowski, kwa tuhuma zilizotolewa dhidi
yake, Vatican imemvua kuwa mwakilishi wa kidiplomasia wa Jimbo Takatifu.
Na
hiyo ndiyo maana alirudishwa Roma mara moja. Hatua hiyo inaelezea jinsi Jimbo la Papa
lilivyojali na kushirikiana na mamlaka katika Jamhuri ya Dominika kushughulikia kashfa.
Jimbo la Papa halikuwa na chochote cha kufichaficha katika kesi hii, bali linaishughulikia
kikamilifu kwa mujibu wa sheria za Vatican , na Papa Francisko yuko makini, akitaka
haki itendeke bila kupendelea upande wowote. Na hivyo Padre Federico Lombardi
alimalizia kwa kuthibitishia tena waandishi wa habari kwamba, Nuncio wa zamani Josef
Wesolowski tangu atuhumiwe, Jimbo la Papa lilimvua hadhi zote za kidiplomasia na kinga
yake, na hivyo anaweza pia kushitatakiwa katika taratibu za mahakama za kawaida za
kiraia.
Taarifa zinasema , Josef Wesolowski anakabiliwa na mashtaka pengine
si tu katika Jamhuri ya Dominika, lakini pia katika taifa lake la kuzaliwa Poland.