2014-08-23 09:38:55

Maaskofu wa Afrika Kusini wahuzunishwa na madhulumu dhidi ya Wakristo Iraq


Baraza la Maaskofu Katoliki la Kusini mwa Afrika, ambalo huunganisha Maaskofu wa Afrika Kusini, Botswana na Swaziland, limekemea vikali vurugu za maonevu na mauaji katikaUkanda wa Gaza na kama ilivyo Iraq ambako Jumuiya za kikristo zimekuwa chambo cha utesaji na mauaji na kufukuzwa kutoka nchi yao.

Taarifa ya Maaskofu iliyotolewa na Askofu Mkuu wa Pretoria, Askofu Mkuu William Slattery OFM, inasema kuwa katika mwezi huu,ambamo Dunia inakumbuka kupita kwa miaka 100 tangu Vita ya Kwanza ya Dunia, ilipoanzishwa, bahati mbaya hata kwa wakati huu , kuna matukio mengi ya kutisha yanayowafanana na ilivyokuwa wakati huo wa vita ya kwanza ya dunia. Kwa maoni ya Maaskofu , inaonekana kwamba, hakuna somo duniai iliyojifunza juu ya ubinadamu wakati wa vita hiyo ya kwanza ya dunia. Kileo, hakuna tena vita , kimetokomea na hivyo mamilioni y awatu kuendelea kuteseka na kuuawa bila huruma, Maaskofu wanasema.

Maaskofu wanataja pia kwamba, sehemu mbalimbali za Afrika, kama ilivyo nchini Iraq na Syria na sasa katika Gaza, zinakabiliwa na hali ya kutisha na kuogofya sana, yenye ushahidi wazi wa kufilisika kwa maadili katika vita vinavyoendelea. Na katika asili yake, kwenye hali ambamo kwa silaha zisizoweza kutambua kati ya wapiganaji na wasiokuwa wapiganaji, na ambapo wenye mamalaka makubwa hufadhaishwa na mtindo wa kipekee wa watu kujitolea mhanga kusheheneza miili yao wenyewe kwa mabomu makali bila woga, hivyo vita vya kisasa vinakuwa na mweleko wa kutisha zaidi kuliko hata ilivyokuwa zamani.

Maaskofu kuwa kwa hiyo, wanatoa ombi kwa serikali ya Israeli na Mamalaka ya Palestina kukomesha vita, kusitisha vurugu na kuacha kuuana. Na pia wametoa wito kwa viongozi , kuwajibika wao wenyewe kaiak kuehdhimu haki msingi za utu wa binadamu na haki za kutofautiana. . Maaskofu wanasisitiza kwamba, amani inawezekana tu kwa kuketi pamoja katiak majadiliano, na kufikia muafaka wa kujenga amani ya kudumu.

Na kwa Wakristo nchini Iraq, Maaskofu wa Kusini mwa Afrika wanasema, ni unyama wa hali ya juu, kuw ana mawazo ya kuwafukuza Wakristu nchini Iraki amba wamekuwa wakiishi ktika nchi hiyo tangu mwanzo wa Ukristo, miaka zaidi ya elfu mbili iliyopita. Maaskofu wameonyesha kujali hali ya mateso kwa Wakristo , na pia kwa ajili ya kuharibiwa kwa majengo ya makanisa ya kihistoria, ambao ni urithi wa Wakristo wote si Wakristuìo wa Iraki tu, lakini dunia yote. Wakitaja kile kinachoendelea Iraki ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Katika tamko lao, Maaskofu wamewaambia watu wa imani zingine , wanaoteseka pamoja na Wakristo kwamba, mioyo yao na maombi pia wako pamoja nao. Na kwamba, wanaheshimu mafundisho mengi ya dini ya Kiislamu, na hasa huduma zao kwa maskini na wahitaji. Na hivyo wanatoa wito kwa Waislamu aminifu ambao wanaamini katika ubinadamu wa kila mtu, wawasihi wale wanaoendesha madhulumu dhidi ya watu wengine wasio waislam , wasitishe ukandamizaji huu wa kutisha, na warejeshe amani kama mafundisho halisi ya dini ya Kiislamu yanavyosema.








All the contents on this site are copyrighted ©.