2014-08-22 09:52:33

Uvunjifu wa amani na utulivu ni hatari kwa ustawi na maendeleo ya watu!


Patriaki Bartolomeo wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodox la Costantinopol katika tamko lake anasema kwamba, hakuna dini wala imani yoyote ile inayoweza kuhalalisha nyanyaso na madhulumu ya watu wasiokuwa na hatia. Kanisa halitakaa kimya na kuona watu wanadhulumiwa na kuteswa; watu wakishindwa kuonesha uvumilivu wa kitamaduni na matokeo yake kusababisha mauaji na mateso ya maelfu ya watu kwa misingi ya chuki za kidini na ubaguzi.

Patriaki Bartolomeo wa kwanza anasema, wananchi wa Iraq kwa sasa wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha, kwani wengi wao wamelazimika kuyakimbia makazi yao bila hata ya kuchukua mambo msingi katika maisha.

Patriaki Bartolomeo wa kwanza anapenda kuungana na viongozi mbali mbali wa kidini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kuomba msaada kwa ajili ya wananchi wa Iraq. Anawataka viongozi wa kidini na kiserikali kuanzisha mchakato wa majadiliano yatakayosaidia upatikanaji wa amani ya kudumu nchini Iraq

NI matumaini yake kwamba, Mwenyezi Mungu chemchemi ya amani na mapendo atawajalia waamini wa dini mbali mbali kuishi kwa amani na utulivu na kwamba, misimamo mikali ya kiimani haina tija wala mashiko!







All the contents on this site are copyrighted ©.