2014-08-21 15:18:43

Yapita miaka 100 tangu kutokea kifo cha St Pius X, Papa mchungaji na Mlezi


Pamoja na mambo mengine Mama Kanisa wiki hii anafanya kumbukumbu ya kupita miaka mia ya kifo cha Mataktifu Papa Pius X. Hitimisho la kumbukumbu hii, itakuwa siku ya Jumamosi ambamo Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican , katika Madhabahu MatakAtifu ya Cendrole ya Riese, katika jimbo la Treviso, hapa Italia, ataongoza Ibada ya misa mahali hapo alizaliwa Giuseppe Sarto, mwaka 1835.

Kardinali Pietro Parolin - katika mahojiano iliyochapishwa na gazeti la la Jimbo la Treviso, na kunukuliwa na gazeti la Vatican, L’ Osservatore Romano, ameonyesha kutambua utumishi unaofanana hasa katika mtindo wa huduma kati ya Pius X na Papa Francisko. Na hasa Kardinali alilenga katika jinsi Papa Pius X alivyojikita si tu katika kupambanua matatizo ya Kisasa, lakini pia juu ya uhai wa kichungaji. Na hivyo kuanzisha ndani ya kanisa, mapema katika karne ya ishirini mwelekeo mpyawamageuzi katika utendaji wa kanisa.

Gianpaolo Romanato, profesa wa historia ya kisiasa katika Chuo Kikuu cha Padova na Mjumbe katika Taasisi ya Kipapa ya Sayansi ya kihistoria, katika mahojiano na Debora Donnini, ameeleza kwamba, kuna kufanana katika utendaji wa kihistoria wa maisha ya kichungaji ya Papa Pius X na Papa Francisko, na hasa katika wazo la kufanya mageuzi kwenye utendaji wa Kanisa.

Baada ya Baraza la Trent la 1588, mengi yalibaki kama ilivyoamuliwa bila kufanya marekebisho hadi miaka ya mwanzo ya 1900, ambamo Papa Pius X, alionyesha nia ya kufanya mabadiliko katika utendaji wa Kanisa. Mawazo yaliyo endelezwa na kuunda Idara za Curia, ikiendelezwa zaidi na Papa Paulo VI na John Paul II,na hata leo, bado ni kunafanyika mageuzi mapya kwa muono wa Papa Pius X, pamoja na mageuzi yaliyofanywa mwaka 1908.

Aidha Profeswa Gianpaolo, ameeleza sababu zilizomsukuma Mtakatifu Pius X, kuwa mpenzi wa kazi za uinjilishaji na katika kuwaandaa watu, kuzamisha maisha yao katika moyo wa Ukristo, inatokana na yeye kuishi maisha ya Padre Parokiani, ambamo aliona mwendelezo wa katekesi kwa waumini , kuwa ni jambo muhimu sana. Kwa Papa Pius X, uinjilishaji na Katekesi, vilipata kipaumbele cha juu katika utawala wake. Papa Pius ni Papa pekee katika nyakati za sasa ambaye alikuwa kwa miaka mingi Padre wa Kanisa dogo na baadaye kutumikia kama Paroko kwa kipindi cha miaka miaka ishirini katika Parokia ndogo ya vijijini. Na hivyo kazi za Kichungaji alizijua vyema, has katika ubunifu wa kichungaji, kwa ajili ya kufikisha kwa watu moja kwa moja, maambukizi ya ujumbe wa Injili kama sehemu ya maisha yake .

Na hivyo, alikuwa mstari wa mbele katika juhudi za kufanya mabadiliko katika liturujia, na mageuzi katika namna za waamini kushiriki katika Ibada za kuabudu, na ukuu wa katekismu na uendelezaji wa ibada ya Ekaristi. Hadi Pius X, taratibu za Ibada za Ekaristi zilifranyika mara chache. Pius X, kwa upande mwingine, alikuza haja ya waamini kupokea Ekaristi Takatifu mara kwa mara na kupunguza umri wa watoto kuanza kupokea communio,akijali kwamba , Ekaristi ni silaha muhimu, kwa muumini katika kubaki thabiti katika Kristo.

Profesa Gianpaolo anamtaja Papa Pius X, kwamba, moyo wa upapa wake, hasa ulilenga katika mageuzi ya ndani ya Kanisa, na katika mfumo wa kichungaji , katika idara za Curia ya Roma na katika uhusiano wa Taasisi za Kanisa na waamini na ushariki wa waamini. Mageuzi ya Kanisa, basi, lilikuwa ni "lengo" kuu katika Upapa wake. Na aliona mageuzi mapya yaliyokuwa yakiendelea katika maisha ya kijamii, yalikuwa ni tishio kubwa kwa uadilifu wa imani. Aliogopa kwamba kupitia mienendo ya mabadiliko ya maisha ya kawaida ya kijamii, pia taratibu yataanza kurarua dhamana ya imani kwa waamini, na hivyo ilikuwa ni vyema Kanisa kutembea na mabadiliko hayo lakini bila kubadili imani kwa Kristo .








All the contents on this site are copyrighted ©.