Imetangazwa Mada ya Ujumbe wa Papa kwa Siku ya 48 ya kuombea amani Duniani (1 Januari
2015).
“Hakuna Mtwana, Wote ni Ndugu ”, ni Mada itakayoongoza Ujumbe wa Papa kwa ajili ya
siku ya 48 ya Kuombea amani duniani, hapo Januari Mosi 2015. Hii ni mara ya pili
kwa Papa Francisco kutoa Ujumbe wake kwa ajili ya siku hii , tangu alipochaguliwa
kuliongoza Kanisa la ulimwengu, March 2013.
Baraza la Kipapa kwa ajili ya
haki na amani , linaeleza kwamba, katika ujumbe wa mwaka ujao, Papa Francisko, anakumbusha
kwamba, wengi wanafikri, utumwa ni jambo la zamani lililopitwa na wakati . Lakini
kumbe, maovu haya bado yako, tena kwa nguvu katika dunia ya leo.
Mwaka jana
Papa katika Ujumbe wake kwa tukio hili la Januari Mosi 2014, ulilenga zaidi katika
baraka za udugu: kwamba, “Uduna Mungu mwenyewe kwa sura na mfano wake Mungu, na hivyo
wote wana hadhi sawa. Lakini kwa bahati mbaya, kuna wachache wanaoiua hadhi hiyo,
na hivyo kuvuruga hata amani yao. Papa alieleza amani, katika ukweli, hupatikana kwa
kutambua ubindamu wa mtu mwingine kwamba ana hadhi sawa. Lakini nyakati hizi zetu,
haki hii hufinyangwa na mambo mengi ya kuchukiza, yenye nyuso za kuwaingiza wengine
katika utumwa mambo leo. Mfano kusafirisha wengine na kuwaingiza katika utendaji
ulio kinyume na hadhi yao, mfano ukahaba, kazi ya sulubu, ungandamizwaji na matendo
mengine ya kitumwa yanayo dharirisha hadi ya utu wa mtu hasa kwa wanawake na watoto.
Hali hizi za kitumwa huonekana katika mambo mengi ya aibu, yanayofanywa na watu binafsi
au vikundi,kwa ajili ya kujipatia faida au utajiri wa harakaharaka, ikiwemo kuzusha
migogoro ya kisiasa, kama inavyosikika sehemu nyingi za dunia, na pia kipeo cha uchumi
kinacho shamirishwa na uovu wa rushwa.
Ujumbe wa Papa unakumbusha utumwa
ni jeraha la kutisha linalo taka kujifunua kwa wazi katika mwili wa jamii ya kisasa,
na ni jeraha kubwa katika mwili wa Kristo! Ili kukabiliana na hali hiyo kwa ufanisi
zaidi , zaidi ya yote kunahiajika kutambua kulinda hadhi ya kila mtu, na pia kuzingatia
thamani yake katika udugu wa binadamu, kama hitaji msingi la kushinda vishawishi vya
ukosefu wa usawa, unaosababisha mtu mwingine mwingine kuwekwa katika hali za kitumwa,
na matokeo yake yanahitaji uwepo wa njia ya ukombozi kwa watu wote.
Na hivyo
Lengo liwe kujenga ustaarabu ulio simikwa juu ya hadhi ya sawa wa binadamu wote,
bila ubaguzi. Kwa hili, pia inakuwa ni muhimu kuwa na mabadiliko mapya katika kazi
zote za malezi, elimu na utamaduni kwa ajili ya jamii, yenye kuongoza katika uhuru
na haki na hivyo katika amani kwa watu wote.
Siku ya Dunia ya kuombea
Amani , ilianzishwa na Papa Paulo VI, na husherehekewa kila mwaka tarehe Mosi Januari.
Ujumbe wa Papa kwa ajili ya siku hii, hutumwa kwa Maaskofu wote duniani na pia kwa
wajumbe wote wa Kidiplomasia wanaowakilisha Jimbo Takatifu , kama ujumbe wa kuanza
mwaka mpya kiserikali.