2014-08-20 13:00:29

Papa Francisko afikwa na msiba!


Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 20 Agosti 2014, amewashukuru wale wote waliomtumia salam za rambi rambi kutokana na msiba ulioikumba familia yake kutokana na ajali ambayo imesababisha Mpwa wake kupoteza mke na watoto wawili. Ajali hii imetokea nchini Argentina. Salam hizi za rambi rambi zimesomwa wakati wa Katekesi yake katika lugha mbali mbali.

Baba Mtakatifu amewakumbusha mahujaji ya wageni waliokuwa wamemiminika kwa wingi mjini Vatican ili kusikiliza Katekesi yake mara baada ya kujerejea kutoka katika hija ya kitume nchini Korea ambako amehudhuria maadhimisho ya Siku ya Sita ya Vijana Barani Asia pamoja na kuwatangaza Mashahidi 124 kutoka Korea kuwa ni Wenyeheri.

Baba Mtakatifu anasema wao katika familia yao walikuwa watoto watano. Kwa sasa ana wapwa zake kumi na sita na kati yao, mmoja wao amempoteza mke na watoto wawili na yeye mwenyewe hali yake bado si nzuri. Anasema hata Papa anafamilia. Amewaambia mahujaji kwamba, ni mshabiki mkubwa wa Timu ya Soka ya San Lorenzo ambayo hivi karibuni ilitwaa ubingwa.

Timu hii anasema, ni sehemu ya utambulisho wake wa kitamaduni. Baba Mtakatifu Francisko amebahatika kusalimiana na wachezaji wa timu hii mmoja mmoja pamoja na kupiga nao picha ya pamoja wakiwa wamebeba Kombe la ushindi.







All the contents on this site are copyrighted ©.