Jitihada za Umoja wa Mataifa katika kupambana na Ebola
Bwana David Nabarro, mtaalam na mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia ugonjwa
wa Ebola ambao kwa sasa umekuwa ni tishio, Siku ya Jumatano tarehe 20 Agosti 2014
anaondoka mjini Washington DC, Marekani kuelekea Afrika Magharibi ili kusaidia juhudi
za kupambana na ugonjwa wa Ebola. Akiwa Afrika Magharibi anatarajiwa kuzungumza na
wananchi, jumuiya na viongozi wa Serikali ambazo zimeathirika kwa ugonjwa wa Ebola.
Bwana David anasema amekwishazungumza na Benki ya Dunia, wataalam wa kudhibiti
na kutibu magonjwa ya mlipuko kutoka Serikali ya Marekani pamoja na wadau wengine,
ilikuhakikisha kwamba, Umoja wa mataifa unawasaidia wananchi wa Afrika Magharibi kukabiliana
kikamilifu na ugonjwa wa Ebola. Akiwa Afrika Magharibi Bwana David anatarajiwa kutembelea
Liberia, Sierra Leone, Guinea na Nigeria.
Hizi ni nchi ambazo kwa sasa zinakabiliwa
na uhaba mkubwa wa wafanyakazi katika sekta ya afya, lakini zaidi kwa ajili ya kuwahudumia
wagonjwa wa Ebola pamoja na kuwatunza wagonjwa wengine pia.