Jumatatu, mara baada ya Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu la Myeong –dong, Baba Mtakatifu
aliekea katika uwanja wa ndege wa Seoul, ambako aliagana na wenyeji wake, Rais Park
Geun-hyne, Nunsio wa papa nchni Korea, Mons. Oswald Padila Maofisa a ngazi za juu
katika wa utawala wa Jamhuri ya Korea Kusini, wakiwalikisha utawala wote mahalia. Papa
aliagwa kwa gwaride la heshima la kijeshi kabla ya kupanda ndege ya Shirika la Korea
kuelekea Roma, akiwa amekamilisha ziara yake ya siku tano nchini Korea Kusini. Jumatatu
hii Papa na ujumbe wake, alitarajia kutua katika uwanja wa ndege wa Ciampino mjini
Roma, saa kumi na mbili za jioni. Akiwa agani alipeleka salaam za matashi mema
kwa Rais a Kila taifa alilopita, ambayo ni Korea China Mongolia Urusi Belarus
Poland Slovakia Austria Slovenia Croatia Italia Kwa Rais w Korea alisema, Mheshimwia
Rais Park Guen-hye , Mimi sasa naondoka Korea kuelekea Roma, Kwa mara ingine narudia
kutoa matashi yangu mema kwako wewe Rais na kwa raia wote na ninawaombea baraka za
Mungu kwenu nyote ajili ya Amani na ustawi wa Rai ya Korea. Kwa Rais wa China
amesema, Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, ninayo heshima
ya kukujulisha kuwa narudi Roma baada ya ziara yangu Korea, napenda kurudia tena kwako
Mheshimiwa na raia wote wa China, matashi mema na naomba Baraka ziwe kwako na nchi
yote ya China. Na akipita katika anga la Mongolia , alipeleka salaam kwa Rais
Tsakhiagiin Elbegdorj wa Mongolia, na kusema, Mheshimiwa Rais naruka juu ya anga la
nchi yako, nikitokea Korea. Napenda kurudia salaam zangu za matashi mema kwako wewe
na raia wote wa Mongolia, nawahakikishia sala zangu kwa taifa la Mongolia. Na
nchini Urusi alisema , Mheshimiwa Rais Vladimir Putin, Rais wa Shirikisho la Urusi
nikiruka juu ya Urusi kutoka ziara yangu ya kichungaji nchini Korea, napenda kurudia
matashi yangu mema kwako na kwa raia wote , na ninawahakikishia maombi yangu kwa taifa
lako. Maneno kama hayo pia ameyatoa kwa mataifa mengine alipita Bielorussia, Poland,
Slovakia, Austria, Slovenia, Croatia , na nchini Italia alimwambia Rais Giorgio
Napolitano , kwamba narejea toka safari ndefu ya Korea , ambako nimekutana na waamini
wengi na uwakilishi wa utawala mzuri wa kupendeza wa Korea ambako kuna ukuaji mzuri
katika yote kiroho na kijamii. Na kwa furaha zote , napenda kutoa kwako wewe Mheshimiwa,
salaam zangu za upendo na kukuhakikishia sala maalum kwa ajili ya mema yote na utulivu
wa taifa zima la Italia, na kwa upendo mkuu nalipa Baraka zangu. .