2014-08-18 11:55:45

Wasalesiani waadhimisha miaka mia mbili ya kuzaliwa Don Bosco


Jumatano ya tarehe 16 Agosti 1815, ikiwa siku baada ya Siku Kuu ya Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni, iliendelea kuwa furaha kubwa kwa familia ya Francesco Bosco na Margherita, kwa John Bosco kuzaliwa.

Kwa ajili ya maadhimisho ya kutimia miaka mia mbili ya kuzaliwa kwa Don Bosco, mwanzilishi wa Shirika la Wasalesiani, Mkuu wa Shirika la Wasalesiani, Padre Angelo Fernandez Artime, aliongoza Ibada ya Misa kwa ni hiyo, katika kituo cha Kiroho cha Colle Don Bosco. Ibada iliyohudhuriwa na familia kubwa ya wasalesiani wake kwa waume , akiwepo pia diwani wa eneo hilo.
Don Artime, katika mahubiri yake, alitaja furaha ya Wasalesiani kwa kuzaliwa kwa mwanzilishi wa shirika lao, furaha ambayo huiishi muda wote, na iliyo huishwa zaidi wakati Don Bosco , alipotangazwa Papa Yohana Paulo 11, kuwa ni Baba na Mwalimu wa Vijana, wakati wa maadhimisho ya kutimia miaka mia tangu kifo chake kilipotokea.
Padre Artime, alirejea maneno ya Injili ya siku akisema, kwao unapaswa kuwa wimbo wa sifa na shukrani kwa Mungu Mkuu, Baba mwenye huruma, kwa kulijalia Kanisa, Mtakatifu Yohana Bosco kama rafiki, ndugu na baba wa vijana.

Homilia ya Padre Artime, iliendelea kukitazama kipaji cha Don Bosco, na kubaini kwamba, ni majaliwa ya Mungu na zawadi kwa Kanisa la ulimwengu, kwa kuwa kupitia kwake mikono ya mama Margaret, Don Bosco aliweza kujenga njia ya urafiki na kuwa walimu mema wa maisha, hatua kwa hatua, na kuchagiza moyo mkuu wa kuwa Mchungaji Mwema, akiyaiga maisha ya Yesu Mwalimu mwema, katika maisha yake ya kila siku, na kuyaeneza mafundisho aliyoyapata toka kwa wazazi wake na kanisa kwa vijana wengine.

Kwamba kijana, Bosco, ambaye ndani ya moyo wake alikumbatia malezi ya Bwana wake kwa msaada wa Mama Mtakatifu Sana Bikia Maria, alifanya kila linalo wezekana, ili kuhakikisha mapenzi ya Mungu yanatimizwa kwa moyo wa furaha ya uchachi na heshima, na kukamilishwa kwa kuuangalia msalaba wa Kristo. Na hivyo kuondoka nyumbani kwao, hakuonekani kama utukutu, bali neema ya Bwana hadi alipompumua pumzi yake ya mwisho.

Don Bosco Don, kwa njia hii anakuwa kioo, baba na mwalimu wa vijana, na katika kuiona ishara ya kudra ya Mungu kwamba, ina msukumo wa kipekee kwa kila kusudi jema.

Padre Artime, alimalizia homilia yake akisema, maadhimisho haya ya miaka mia mbili ya kuzaliwa Don Bosco, , inakuwa ni nafasi ya kipekee na wakati huohuo ni changamoto inayodai maisha ya upendo kupitia huduma ya elimu na huduma za kitume kwa wavulana na wasichana wa ulimwengu huu, kuwawezesha kutambua kwamba maisha yao ni zawadi ya Mungu, kwa ajili yetu na ni tendo la Roho Mtakatifu, katika kila mmoja wao , na katika kushirikishana ndoto zao, matarajio, na matatizo. Vijana wakisaidiana kwa kushirikishana uzoefu, waelimishaji wa , wavulana na wasichana, walio tayari kusimama kando ya wahitaji, katika safari ya maisha, kwa sababu, kama Don Bosco, pia wanataka kuwa na furaha sasa na hata milele.
Na hivyo waanza mwaka wa Jubilee , kwa furaha kuu na kumtukuza Mungu kwa majaliwa ya kuzaliwa Don Bosco.Na pia kwa ajili ya kugundua mahali ilipo furaha ya kweli inayozaliwa kutoka katika kazi za nyingi na pengine nzito za kujituma , kama ilvyo kwa Mkulima kutoka jasho wakati akiitumikia aridhi na baadaye huvuna matunda tele kwa furaha.








All the contents on this site are copyrighted ©.