Baba Mtakatifu Francisco, kwa barua yake ya kitume ya Julai 26, 2014, amempeleka
Kardinali Justin Francis Rigali, kuwa mjumbe wake maalum kwa ajili ya sherehe za kutimia
miaka 250 , mji wa St Louis Marekani, maadhimisho yatakayofanyika rasmi, tarehe 24
Agosti 2014, kwa Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu jipya la Saint Louis (USA).
Barua
ya Papa kumteua Kardinali Rigali, ilichapishwa tarehe 26 Julai na kunukuliwa na
gazeti la Vatican L'Osservatore Romano, ikimtaja Kardinali Francis Justin Rigali,
Askofu Mkuu mstaafu wa Philadelphia (USA), kuwa Mjumbe Maalum wa Baba Mtakatifu, katika
Ibada ya Misa ya Ekaristi, iliyopangwa katika Kanisa Kuu mpya ya Saint. Louis (USA)
Agosti 24, 2014, kwa nia ya maadhimisho ya miaka 250 ya mwanzilishi wa mji St Louis.
Wengine walioteuliwa kuandamana na Kardinali Rigali ni pamoja Mons Breier J. Henry,
Paroko wa Parokia ya Malaika Raphael na pia Mwenyekiti wa Baraza la Makasisi Mons.
Leykam John Jpia Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Kupaswa Habari na Mshauri katika
Baraza la moja ya Makasisi.
Aidha Baba Mtakatifu Francisko, katika ukurasa
wake wa Tweet @pontifex, ametoa ombi maalum kwa ajili ya Iraki, ambamo ameomba,”
mbele ya ghasia na fujo nyingi Iraki , tudumu katika sala na ukarimu” . Ujumbe
wa Papa pia unatutaka kuandamana na Mjumbe wake nchini Iraki , Kardinali Fernado Filoni
, ambaye kwa wakati huu anatembelea Baghdad. Jumapili aliweza kukutana na jumuiya
mbalimbali za kidini katika eneo lililokumbwa vibaya na machafuko la Yazid, ghasia
za utumiaji silaha zinazofanywa na wanamgambo wa Kiislamu wa serikali ya Kiislamu.
Taarifa inabaini, Mjumbe binafsi ya Baba Mtakatifu nchini Iraki , Kardinali Fernando
Filoni, akifuatana na Patriaki Sako, Mjumbe wa Kitume Iraki, na Maaskofu wa ndani,
walikutana na viongozi wa kisiasa wa Utawala wa Mkoa wa Kurdistan na kuwatembelea
wakimbizi Wakristo, Yazidis na mikoa mingine, Duhok na Erbil.
Baada ya kusikia
na kuona maafa na mateso ya familia nyingi ambazo ziliondoka katika vijiji vyao kuacha
nyumba na mali zao, hususani katika Mosul, na eneo la uwanda wa Ninawi na Sinjar,
wote wameungana na ombi lililotolewa na Patriaki wa Kaldayo ya Babilonia, kuitaka
Jumuiya ya Kimataifa , na hasa kwa nchi na mashirika ya kimataifa yenye kuwa na mamlaka
zaidi ya uwajibikaji wa kimaadili, kuingilia kati mara moja, na kufanikisha msaada
wa ubinadamu wa kidharura, maji, chakula, dawa, huduma za afya, nk. Na tatu ni kutoa
ulinzi wa kimataifa kwa vijiji hivi kwa kuhamasisha familia kwa kurudi majumbani mwao
na kuendelea maisha yao ya kawaida kwa usalama na amani. Katika maeneo hayo, Kardinali
amesema kote watu wanapiga ukelele wa kuomba msaada wa kusitishwa ghasia na wana hamu
yakurudi makwao.