2014-08-17 11:38:02

Mateso ya Kanisa la Korea ni mfano wa kuigwa katika uinjilishaji - Korea


Jumapili Papa Francisko akiwa katika madhabahu ya Mama Yetu wa Haemi , ambayo yalijengwa kwa heshima ya kuwakumbuka Wakristu waliouawa karne ya XIX, Kardinali Osward Gracias, Mwenyekiti wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Barani Asia alitoa hotuba kwa ajili ya kumkaribisha Baba Mtakatifu Francisko kuzungumza na Maaskofu Katoliki kutoka Barani Asia.

Katika salaam hizo Kardinali Osward alikumbuka mkutano wa kwanza wa Maaskofu wa Asia na Papa Paulo VI, uliofanyika Ufilipini mwaka 1970 na kufuatiwa na Maamuzi ya Maaskofu wa Asia, kuunda Shirikisho la Baraza ya Maaskofu Katoliki Barani Asia, (FABC), kama chombo cha kuwaunganisha pamoja kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika utendaji wa kazi za kichungaji na changamoto zinazokabili bara hili kubwa, lenye utajiri mwingi wa tamaduni tofauti, kama yalivyoundwa pia mabaraza mengine kama vile CELAM, SECAM, ECC kwa baraka za Papa Paulo VI.

Rais wa FABC, kwa muhtasari alieleza mafanikio ya Baraza na Tume, na shughuli muhimu, wanazo endelea kutekeleza hadi leo hii. Kwamba FABC, imekuwa ikitoa msaada endelevu kwa Kanisa barani Asia kupitia Ofisi zake na mipango ya malezi na uhamasishaji wa kichungaji kwa Maaskofu, Watalaam na wote wanaohusika katika sekta hii. Na bila ya kusahau utendaji wa FABC, katika suala nyeti la uinjilishaji wa kanisa Asia, lengo kuu la kuanzishwa kwa FABC, leo hii huunganisha Mabaraza ya Maaskofu Katoliki 19 ya nchi 27, na kukiwa na wabia wengine wanachama 9 wa Makanisa yasiyokuwa bado na Mabaraza ya Maaskofu.

Katika salaam hizo, Kardinali Gracias, pia alirejea moyo wa umisionari wa Kanisa la Ulimwengu katika mtazamo wa bara la Asia, ambako kunaishi karibia asilimia sitini ya watu wote duniani. Pia akilitaja kuwa bara lenye kuwa na idadi kubwa ya watu vijana. Na hivyo, kwa namna mbalimbali bara la Asia kwa hakika ni msingi wa hali ya baadaye ya dunia na pia kwa kanisa.

Aliendelea kufafanua kwamba, Kanisa Asia, linatambua maeneo matatu katika maendeleo yake, majadiliano na tamaduni, majadiliano na maskini na majadiliano na dini. Aidha kwa jinsi utandawazi ulivyo athiri Asia, licha kwamba, Watu Asia wana asili ya kuzingatia maadili ya dini na utamaduni, aambavyo kwa wakati huu vijana wanapokonywa urithi huo na utandawazi, na kumezwa na moyo wa kutomjali Mungu. Na pia mahusiano ya familia nyakati za nyuma yalichukuliwa kuwa na umuhimu wa kipekee lakini sasa polepole urithi huo unamomonyoka. Tena, wakati roho za waasia, ziliyachukulia maisha kama jambo takatifu, lakini sasa vitisho dhidi yake vinazidi kuongezeka katika njia mbalimbali. Pamoja na hayo yote, watu wa Asia, bado wanapenda kuwa jamii ya furaha, ingawa kuna kishindo cha hisia hisia kali ya ubinafsi.

Matokeo yake ni heshima ya ndoa na familia kushambuliwa, talaka iliyokuwa mwiko kutolewa siku za nyuma sasa ni jambo la kawaida. Harakati dhidi ya maisha imeongezeka na kutishia maisha yenyewe katika njia kadhaa, kama vita vya kikabila, machafuko ya kiraia kati ya jamii, kukandamiza vurugu ya imani za dini; tishio kutisha ya maisha ya watu wanaoishi katika mazingira magumu, watoto wasiozaliwa bado. Na hata euthanasia.

Hata hivyo Kardinali alibaini, Roho Asia bado inatafuta maisha ya furaha katika jamii, licha ya kugandamizwa na hisia kali ya ubinafsi, ukosefu wa kuwa makini na kila mmoja na kutofautiana katika mahitaji, hasa ukosefu wa roho ya ukarimu na uwazi, ambayo awali ilikuwa ni jadi asili katika jamii zote Asia . Sasa wamepoteza roho ya upendo na maridhiano kati ya madhehebu, kama wanavyoshuhudia ongezeko la mashambulizi dhidi ya dini. Katika baadhi ya nchi, mateso ya Wakristo yameongezeka, na wakati mwingine ubabe wa kidini na itikadi, hutafuta kulazimisha hata mamlaka ya kisiasa juu ya makundi ya kidini.

Kardinali Gracias , alikamilisha salaam zake za Papa , kwa kutoa maelezo mafupi juu vipengele maalum, katika mazingira ya Asia: kwamba, kwa Waasia, dini ni jambo muhimu linamtaka mtu kufuata mafundisho au utii kanuni na sheria. Kwa hiyo, mfuasi wa Yesu, anapaswa kuyatolea maisha yake yote katika kutii Injili kama ilivyokuwa kwa Yesu Mwenyewe katika maisha yake, mateso yake, kifo na ufufuo wake. Kwa namna hiyo Makaburi ya Bikira Maria huvutia watu wa dini zote, kutolea heshima zao, kwa ajili yake.

Mawazo ya Waasia hufarijiwa zaidi kwa sala na tafakari makini, na hivyo huweza kujenga utajiri wa maridhiano na watu wengine kushiriki pamoja. Na kuna ukuaji mkubwa wa mawasiliano, ambayo wanachukulia kama ni zawadi ya Mungu katika kueneza habari njema. Na hivyo ni kazi ya kanisa kuelimisha vijana hasa kwa matumizi ya mapya ya vyombo vya habari.

Na kwamba katika bara hili kubwa la Asia, idadi ya Wakristu ni ndogo, karibu katika nchi zote. Na wanatoa sifa kwa Wakristo wa Korea katika jukumu la Uinjilishaji kwamba ni mfano wa kuigwa na makanisa mengi ya Asia. Na wanatumaini, wataendelea kuguswa na mateso ya kanisa la Korea, wakati watakapo rudi majimboni mwao.








All the contents on this site are copyrighted ©.