Utume wa walei una thamani kubwa katika maisha ya kanisa!
Hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko kwa Viongozi wa Utume wa Walei, imetazama hasa
thamani ya karama mbalimbali katika shughuli za kitume ambazo huimarisha maisha ya
Kanisa nchini Korea. Amesema kwamba, karama hizi huonyesha kwa hakika, uwepo wa
upendo wa Mungu katika miito na kwa wengine, ni ishara ya kuonekana ya uwepo wa Ufalme
wa Mungu.
Lakini Papa alibainisha, ni tu iwapo ushuhuda utakuwa na furaha
ya kuvuta wanaume na wanawake kwa Kristo; na kwamba furaha hiyo, ndipo inakuwa ni
zawadi inayolisha maisha ya sala, tafakari kwa Neno la Mungu, maadhimisho ya sakramenti
na maisha ya jamii. Papa ameeleza mtindo wa maisha, kulingana na viapo vya usafi
wa moyo, umaskini na utii, unakuwa ni ushuhuda wa furaha kwa upendo wa Mungu, uliosimikwa
imara juu ya mwamba wa huruma yake.
Katika mkutano huu wa walei, uliohudhuriwa
na wajumbe wapatao 150, ulilenga zaidi katika historia ya kanisa nchini Korea. Papa
amesema, Kanisa la Korea, lina utajiri mkubwa wa imani iliyoachwa na wahenga waamini
ambao walikuwa ni Wakristo wa kawaida. Kanisa nchini Korea ni mrithi wa imani ya
vizazi vya watu wa kawaida ambao waliweza kuendeleza upendo wa Yesu Kristo katika
ushirika na Kanisa, licha ya uhaba wa makuhani na tishio la mateso makali.
Papa
alirejea uthabiti wa imani ya Mwenye Heri Paulo Yun Ji-chung na mashahidi wengine
waliotangazwa katika Ibada ya Misa Jumamosi hii, kwamba, wanawakilisha sura ya ajabu
ya historia ya Kanisa. Wao walitoa ushuhuda wa imani si tu kwa njia ya mateso yao
hadi kufa, lakini pia na maisha yao ya upendo yaliyo oonesha mshikamano miongoni mwao
kama jamii ya Kikristo, na hivyo kuwa mfano wa upendo kwa jamii yote.
Papa
aliendelea kusema leo kama siku zote, Kanisa linahitaji walei kuwa shahidi wa kuaminika,
ili ukweli kuokoa wa Injili, uonekane katika misingi ya maisha ya kawaida katika kujenga
familia ya binadamu katika umoja, haki na amani. Papa Francis anasema kuwa, Kanisa
la Mungu, ni moja tu , ambamo kila Mkristo aliyebatizwa ana jukumu muhimu katika hija
hii ya kiroho.
Aidha Papa aliangalisha katika zawadi ya vipaji mbalimbali
kwa walei, waume kwa wake, katika kutimiza utume wao mbalimbali, akisema, ina maana
ya kukuza utume wa Kanisa katika kuhakikisha kwamba, ujumbe wa Neno la Mungu, unajipenyeza
na kukamilishwa kwa Roho wa Kristo, hadi ujio wa Ufalme wake.
Papa ameonyesha
kutambua kwa namna ya pekee, jinsi kazi za vyama vingi vya walei , hushiriki moja
kwa moja katika shughuli na huduma kwa ajili ya maskini na wahitaji, hasa waliotupwa
pembezoni na jamii. Na kwamba imani husambaa zaidi kupitia mshikamano halisi wenye
upendo na udugu kwa ndugu zetu wake kwa waume, bila y akujali tofauti za utamaduni
na hali ya kijamii, kwa sababu katika Kristo "hakuna Mgiriki na Myahudi".
Hata
hivyo Papa alionya kusaidia maskini ni jambo jema, lakini haitoshi. Ni vyema kuzidisha
juhudi katika maendeleo ya binadamu, kwa lengo kwamba, ili kila mtu, mke kwa mme,
aweza kujua ukweli kwamba, furaha ya maisha yanayotokana na hadhi ya kupata mkate
wa kila siku, hutoka kwa Mungu mwenyewe.
Papa ameonyesha kutambua mchango
wa thamani unaotolewa na wanawake Wakatoliki wa Korea utume wa Kanisa, kama mama wa
familia, makatekista na walimu, na kwa kupitia huduma zingine mbalimbali. Alisisitiza
umuhimu wa ushuhuda unao tolewa na familia za Kikristo. Amesema, wakati huu wa mgogoro
wa maisha ya familia, jamii ya Kikristo, imeitwa kutoa msaada kwa wanandoa na familia
katika kutimiza kazi yao katika Kanisa na jamii. Familia ni taasisi msingi katika
jamii na shule ya kwanza kwa watoto kujifunza maadili ya ubinadamu na maadili ya
kiroho, ambayo msingi wa wema, uadilifu na haki katika jamii zetu.
Papa
ametoa wito kwa walei kuendelea kukuza katika jamii yao, malezi adilifu kupitia udumishaji
wa taratibu za kutoa katekesi kwa ajili ya mwelekeo chanya wa kiroho na uwepo wa
kishawishi kamili cha kichungaji na ufahamu wa kutambua vipaji na karama katika kulitumikia
kanisa katika umoja na katika roho ya kimisionari. Papa amesema , mchango wa walei
ni muhimu, hata kwa ajili ya uwepo wa kanisa, kata kwa siku za baadaye si nchini Korea
tu lakini Asia yote katika kugawana zawadi za kiroho.