Maombi kwa ajili ya Wakristo Wateswa wa Ulaya iliyowekwa pembezoni
Ijumaa hii Agosti 15, ambamo Kanisa limeadhimisha Siku Kuu kubwa ya Bikira Maria kupalizwa
mbinguni, nchini Italia, Kanisa limetolea sala zake kwa nia ya kuombea Wakristo wote
wanaoishi katika hali ngumu za mateso kwa ajili ya imani yao. Baraza la Maaskofu
la Italia( CEI) lilitangaza nia hii, kama sehemu ya kutoa jibu, lenye kukubaliana
na wito wa Papa Francisko, katika kukabiliana mateso kwa Wakristo leo hii , kama ilivyokuwa
katika karne ya kwanza. Na hivyo, CEI ilitoa mwaliko kwa jumuiya zote za Kanisa kujiunga
katika sala kama ishara halisi ya ushiriki na wote wanaoteswa na ukandamizaji mkali.
Ujumbe wa Baraza la Maaskofu la Italia CEI, unasema, "Hatuwezi kukaa kimya hasa
mbele ya" Ulaya ya yetu, inayo raruliwa na kubadilishwa, na kuwa na upofu na ububu
mbele ya mateso ambayo leo, waathirika ni amia ya maelfu ya Wakristo. haya yameelezwa
na Katibu Mkuu wa CEI, Mons. Nunzio Galantino, ameeleza wakati wa mahojiano na Marco
Guerra, wa Redio Vatican.
Na kwamba kutokana na hali hizi za kusikitisha na
kutisha wanazoziishi Wakristo ktiak baadhi ya maeneo, kuna haja kupaza sauti na kusema
sasa basi yatosha, si tu barani Ulaya, lakini pia katika mataifa mengine, kama ilivyo
huko Yazidis Iraq, Syria, Nigeria na kwingineko. Ni kuwa na mwamko zaidi katika kuweka
wazi zaidi maamuzi juu ya suala hili, kutokana na umuhimu wake wa kutotumia nguvu
katika kuwaondoa katika mateso ndugu zetu hawa, kaka na dada zetu wanaoteseka na
hasa wale wanaoendelea kuvumilia yote na kudumu na imani yao.
Kwa mujibu
wa maelezo ya Mons, Galantino kwa ujumla, Kanisa nchini Italia limeonyesha mshikamano
mzuri na Wakristo wateswa hasa wanaoteseka Iraki, ingawa jawabu la suala hili si sawa
kwa sehemu zote , kuna maeneo mengine ambayo kweli yanahitaji msaada wa kihali hasa
wale waliokimbia na sasa wanaishi katika kambi, au katika majengo ya taasisi wanakoona
ni salama zaidi kwa maisha yao kama ilivyo Samir, katika Parokia ya Mtakatifu Joseph,
ambao wameomba msaada moja kwa mojaNa akizungumzia juhudi za kusitisha ukatili dhidi
ya makundi madogomadogo ya kidini anasema, kwa maoni yake, awali ya yote, ni kupata
taarifa za yote yanayoendelea, kujua watu wote wanafanya nini na kwa nini chuki hii
ya mauaji na mateso kwa watu wasiokuwa na hatia. Na hivyo Wakatoliki wa Italia , tangu
siku ya leo Agosti 15, kwa namna mbalimbali wanatafuta kupata ufahamu hata zaidi juu
ya madhulumu haya kwa Wakristo. Na katika uwezo wake , CEI tayari imetenga fedha,
kwa ajili ya kushughulikia tatizo hili. Maaskofu wamepania kweli kusitisha chuki
hii ya mauaji, hivyo wanaitahadharisha dunia nzima, itoe angalisho makini si tu katika
nchi za Magharibi, lakini na kwingineko dhidi ya janga hili. Na Kardinali Bagnasco,
Rais wa CEI, anasema, sala ni tendo la kwanza muhimu linalowaunganisha na waamini
wateswa na wahitaji wote kwenye parokia na vigango vyote vilipo. Na hivyo kwa pamoja
Kanisa nchini Italia lilitangaza tarehe 15 Agosti, iwe siku maalum ya kuugana kiroho
na kihali na watu wote wanaoteseka kwa sababu ya imani yao. Ameeleza haya na kutaja
jinsi Baba Mtakatifu Francisko anavyoumizwa na taarifa za madhulumu haya, na kulazimika
kukemea na kuitaka jumuiya ya kimataifa iingilie kati, kusitisha dhuluma hizi.