2014-08-15 11:58:58

Afrika watoto kuongeza mara mbili ifikapo mwaka 2050


Kwa mujibu wa Ripoti mpya ya UNICEF ya makadirio ya kizazi kwa mwaka 2030, iliyozinduliwahivi karibuni, juu ya viwango vya uzazi na ongezeko la wanawake walio katika umri wa kuzaa, inaeleza kuwa , katika kipindi cha miaka 35 ijayo, karibu watoto bilioni mbili watazaliwa Afrika, na wakazi wake wenye umri chini ya miaka 18, wataongezeka kwa theluthi mbili. Makadirio hayo yanaonyesha kuwa ifikapo mwaka 2050, idadi ya watoto wanaozaliwa itakuwa zaidi ya 40% ya watoto wote wanaozaliwa, takriban 40% ya watoto wote duniani watakuwa barani Afrika.


Ripoti hiyo ya UNICEF juu ya uzazi, inatahadhari bara la Afrika, kuanza kujenga mkakati wa uwekezaji kwa watoto, wenye kuruhusu bara na dunia, kuvuna faida ya mpito ya idadi ya watu.

"Ripoti hii ni kichocheo kwa ajili ya mazungumzo katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa juu ya watoto wa Afrika," amesema Leila Gharagozloo-Pakkala, Mkurugenzi wa UNICEF, Kanda ya Kusini mwa Afrika. Amesisitiza uwekezaji katika watoto, hasa juu ya afya, elimu na ulinzi - Afrika utawezesha kutoa utambuzi zaidi juu ya faida za kiuchumi na awali ya yote, uzoefu na mikoa mingine na nchi ambayo yamekuwa na mabadiliko katika idadi ya watu.


Na Manuel Fontaine, Mkurugenzi wa UNICEF Kanda ya Afrika Magharibi na Kati, amesema Mpango msingi wa haki na sera za watoto ziweze kusaidia kutoa maamuzi ya kuwezesha watoto kubadili bara la Afrika na kuvunja mzunguko wa lindi la umaskini na ukosefu wa usawa. Na ameonya iwapo uwekezaji kwa watoto hautakuwa kipaumbele barani Afrika, basi bara litaendelea kuwa na uwezo duni katika uvunaji wa faida kamili ya mpito wa idadi ya watu katika miaka ijayo.








All the contents on this site are copyrighted ©.