2014-08-11 11:44:25

Salam za rambi rambi kutokana na ajali ya ndege Iran


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kwa Askofu mkuu Ignazio Bedin, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Iran kufuatia ajali ya ndege ya abiria iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya arobaini, Jumapili tarehe 10 Agosti 2014.

Baba Mtakatifu anasema amepokea taarifa ya ajali hii kwa masikitiko makubwa na kwamba, anamwomba, amfikishie salam zake za rambi rambi kwa ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu.

Katika ujumbe huu ambao umetiwa sahihi na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, Baba Mtakatifu anapenda kuwafariji na kuwapatia baraka na amani wote wanaoombeleza msiba huu mzito.







All the contents on this site are copyrighted ©.