2014-08-09 08:39:44

Mwenyezi Mungu, watie shime wananchi wa Iraq ambao wanakosa mahitaji yao msingi kwa sasa!


Mashambulizi yaliyokuwa yanafanywa na Jeshi la Jihadi, Kaskazini mwa Iraq yamesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao, kiasi cha kuwafanya Wakristo wengi kuyakimbia makazi yao. Hali inazidi kuwa ngumu kwa wakati huu, ambapo Marekani imeamua kupambana na Jeshi la Jihadi, kwa kujielekeza katika ngome za majeshi haya, hasa katika eneo la Makhmur.

Taarifa za kijeshi zinasema kwamba, Marekani itaendelea kushambulia maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu na Jeshi la Jihadi, kutokana na mwelekeo huu hali imekuwa tata zaidi huko Iraq.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake wa tatu, alioutoa Ijumaa usiku tarehe 8 Agosti 2014 anamwomba Mwenyezi Mungu, aweze kuwatia shime wananchi wa Iraq ambao wanateseka kwa wakati huu kwa kukosa mahitaji yao msingi.







All the contents on this site are copyrighted ©.