Wakristu daima hubaki katika giza nene la mashambulizi ya Boko Haramu
Mashambulizi mapya Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, yanayo fanywa na Waislamu wenye
msimamo mkali wa kikundi cha Kiislamu Boko Haram, ni jinamizi lenye kitisho kikali
kwa wakazi wa eneo. Hivi karibuni watu wengi wasiokuwa na hatia wameuawa katika mji
wa Gwoza na watu wengi wengi kulazimika kukimbilia kwa Cameroon. Aidha katika wiki
za karibuni, mashambulizi mapya juu ya jamii ya Kikristo, kama yale yaliyofanyika
Jumapili, Julai 27,katika shambulio la msichana kujilipua mwenyewe katika Parokia
ya Mtakatifu Charles mjini Kano, na kuua watu wanne, ni mambo ya kuogofya sana.
Kardinali
John Onaijekan, Askofu Mkuu wa Abuja, akizungumza katika mahojiano na Radio Vatican
, juu ya dhuluma hizi hizi amesema, mashambulizi iwe yale yanayofanywa na moja kwa
moja na Boko Haram, au yale ya kujitolea mhanga, au yale ya kuweka mabomu katika
magari kulipuka, pamoja lakini lile la msichana kujiua baada ya kukaa na bomu ndani
ya nguo zake kwa muda mrefu, ni jambo lililoshtua watu wote wenye mapenzi mema na
hivyo limewatia jamii wasiwasi, jinsi mtu anavyoweza kukwepa uhalifu huu.
Na
kwamba kwa ujumla, kwa wakati huu Wakristo, hasa katika eneo la Kaskazini , wanaishi
kwa hali ya woga na mashaka makubwa. Na wanatambua wazi kwamba, makanisa ni malengwa
na hivyo daima sasa wanajitahidi kwa kadri wanavyoweza kujilinda, lakini hawawezi
kuwa na uhakika wa usalama wao mia kwa mia. Kwa mfano, hakuweza kufikiria kwamba
msichana anakuja kanisani, anaweza kuwa amevalia mabomu na kujipua mhanga. Na hili
limekuwa ni fundisho la kuchukua hatua mpya, cha kumchunguza kwa makini kila anayepita
katika lango la Kanisa kuu, ingawa ni usumbufu. Kardinali anasema Wakristo wa Nigeria
ni sehemu muhimu ya jamii ya taifa la Nigeria. Bahati mbaya sasa wanateseka mashambulizi
haya, ambayo si tu kwa Wakristo lakini pia kwa watu wengine ikichukuliwa kwamba mashambulizi
pia hufanywa pia katika masoko, taasisi za serikali na maeneo mengine ya umma na
binafsi.
Akizungumzia juhudi serikali ya Nigeria kukabiliana na maasi
haya anasema , ingawa serikali hutangaza kushinda vita dhidi ya Boko Haram, lakini
matokeo yake hayaonekani hivyo, kwa sababu Boko Haram wanaendelea kushambulia na
kuwa kitisho katika jamii. Baada ya karibu mwaka wa utawala wa kidharura, inashangaa,
bado upinzani unaendelea na machafuko na kuleta majanga. Ni lazima kuwa na uhakika
kwamba serikali ni kweli inatenda kwa nguvu, lakini kwa bahati mbaya inaonekana kuwa
na wasiwasi mwingi katika ngazi ya kisiasa, na hasa ikizingatiwa kwamba mwaka ujao
ni mwaka wa uchaguzi. Katika magazeti habari ya Boko Haram ni tu mistari michache
katika gazeti; habari ya ukurasa wa kwanza, daima ni ni habari za kisiasa, zinazowahusu
wakubwa. Matukio ya mashambulizi yanayofanywa na boko haram hupewa nafasi kidogo sana.