Ujumbe kwa Siku ya Wenyeji Kimataifa kwa Mwaka 2014
Jumuiya ya Kimataifa tarehe 9 Agosti 2014 inasherehekea Siku ya Wenyeji Kimataifa
kwa kuangalia kwa namna ya pekee haki msingi za binadamu kama njia ya kujenga jamii
shirikishi. Sheria nyingi za kitaifa na kimataifa zinachota utajiri wake kutoka katika
Tamko la Haki Msingi za Binadamu lililotolewa na Umoja wa Mataifa.
Lakini,
Jumuiya ya Kimataifa bado ina safari ndefu inayopaswa kutekelezwa kwa kusimama kidete
kupambana kufa na kupona na umaskini unaowaandama wenyeji wengi, kiasi hata cha kubaguliwa
na kutengwa katika maamuzi ya kisiasa na kiuchumi. Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku
ya wenyeji kimataifa kwa mwaka huu ni "Tuondoe kinzani: tutekeleze haki msingi za
wenyeji".
Watu hawana budi kujifunga kibwebwe katika kupambana na ubaguzi,
kwa kujenga na kudumisha utamaduni wa kuheshimiana, kulinda na kuendeleza urithi wa
kimataduni unaopatikana miongoni mwa watu.