Shikamaneni na watu waliotikiswa kwa ugonjnwa wa Ebola!
Baraza la Makanisa Ulimwenguni limeguswa sana na hali ya hatari iliyojitokeza Afrika
Magharibi kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa umekuwa ni tishio
kwa afya ya umma na kwamba, una madhara makubwa kwa wananchi wanaoishi Afrika Magharibi
kwa sasa.
Ugonjwa wa Ebola ni hatari kwani haubugui wala hauchagui, linasema
Baraza la Makanisa Ulimwenguni katika taarifa yake. Baraza hili linazihimiza Serikali,
Makampuni binafsi na wataalam wa wafya kushikamana kwa hali na mali katika kudhibiti
kuenea kwa ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi.
Taasisi za afya zinazomilikiwa
na kuendeshwa na Makanisa katika maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa wa Ebola, yawe mstari
wa mbele kuwasaidia waathirika kwa kutambua unyeti wa ugonjwa wenyewe! Baraza la Makanisa
Ulimwenguni linaendelea kuwakumbuka wote waliotikiswa kwa ugonjwa wa Ebola katika
sala na maombi yake!