2014-08-08 11:02:38

Kunahitajika hekima mpya na nguvu mpya kulinda familia


Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Familia, Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Alhamisi, alijiunga na kulihutubia kongamano la Kimataifa juu ya Familia linalo fanyika mjini Panama, kwa siku tano 04-09 Agosti kama ilivyoandaliwa na Baraza la Kìbara la Maaskofu Katoliki (CELAM), katika mtazamo wa kushiriki katika Sinodi Maalum juu ya familia, iliyo itishwa na Papa Francisko kwa mwezi wa Oktoba. Kazi za Kongamano hili zinalenga katika mada "Familia na maendeleo ya kijamii kwa maisha kamili na usharika wa kimisionari.

Alhamisi, Agosti 7 Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Familia, aliangalisha kwa upande mmoja katika kuchambua fursa na changamoto ya familia katika bara la Amerika ya Kusini , kwa ajili ya ufanikishaji maendeleo ya kijamii nchini, kwa upande mwingine, alionyesha matumaini yake kwamba, Kongamano litaweza kukamilika na mchango thabiti katika masuala ya kiuchumi na kisiasa ya familia, hasa katika kuweka msisitizo mpya, juu ya thamani ya kijamii na kipaumbele kwa hayo, kama chanzo cha maendeleo ya jamii. Tumaini jingine ni uwezekano wa "ushawishi wa sera kwa ajili ya familia, ili iweze kuwa kipaumbele katika ajenda za serikali.

Katika mtazamo wa hotuba hiyo ililenga zaidi katika haki ya familia kama moyo wa maendeleo ya mtu na jamii ya wanadamu, Askofu Mkuu Paglia ameonya kwamba, ​​Familia ni upeo huduma kwa maisha kamili na ushirika kimisionari, na hivyo iwapo kuna mapenzi ya kuendeleza njia ya halisi za maendeleo ya binadamu, matarajio ya familia ni muhimu. Awali ya yote, kwa sababu familia ni aina ya kijamii ambayo mna uhusiano imara ya binadamu. Askofu Mkuu Paglia, alielezea aina mbili za uhusiano. Nini uhusiano kati ya jinsia zote (wanaume na wanawake) na vizazi ( baba- mama –watoto ). Alisema kimaumbile wote wanasifa tofauti zisizoweza kubadilika. Lakini kifikra bahati nzuri Muumba alifanya wote kuwa sawa, na hivyo utengano wa kifikira ni ubinafsi uliopo katika wakati wetu, ambao hugandamiza misingi ya bora ya kujitawala na uhuru katika wazo la 'kiasi' na usawa na haki za binadamu. Katika familia, tofauti za maumbile ni jambo la heshima lisilo na mbadala. Aidha, katika dunia ambapo uchaguzi umekuwa, kwa bahati mbaya, mara nyingi jambo la muda, familia imebaki kuwekwa katiak hali ngumu na nafasi ya uhusiano wa nguvu na imara , kuathiriwa sana, katika mema na mabaya, katika maisha ya kila ya mwanafamilia.

Askofu Mkuu Paglia anaendelea kusema, na hivyo katika familia baadhi hupoteza maana ya familia, kutokana na kukosekana kwa utulivu, kama ilivyo katika muktadha wa jamii. Kwa maana hii, familia ni si tu rasilimali lakini pia ni chanzo cha maisha kinacholisha uwepo wa jamii mbalimbali bila kuharibu tofauti. Baba sawa na mama mwenyewe ina maana umoja katika wengine, upendo bila upendeleo. Kwa bahati nzuri, mtoto angalau mpaka sasa kwa wengi , anazaliwa bila kuchaguliwa kama mbegu ya karanga. Na watoto hawana namna ya kuchagua wazazi wao. Familia hivyo, bado katika dunia hii, ambapo jambo la thamani katika uchaguzi wa mtu binafsi, kama vile wigo wa zawadi ya mmoja kukubaliana na mwingine ishara ya uwepo wa Maongozi mengine yaliyo nje ya binadamu. Rais Paglia pia alibaini ongezeko la idadi ya watu katika ulimwengu, wanaochagua kuishi peke yao(singles), ambalo katika muda mfupi sana idadi yao imeongezeka kwa kasi. Hitimisho ni wazi, matokeo yake ni dhahiri kuwa tabia hii ya ubinafsi, ina mwelekeo wa kuathiri jamii na kuwa na familia dhaifu. Haya ni .matunda machungu ya utamaduni ubinafsi wenye kuvamia kila jambo katika maisha. Askofu Mkuu alihitimisha hotuba yake, kwa kuwakumbusha washiriki wote , juu ya matarajio ya Sinodi ya pili ya Maaskofu juu ya familia, kwamba, itaweza kupata majawabu yanayofaa katika kukabiliana na hali ngumu za kitamaduni na kisiasa zinazo zonga uongofu wa kiroho na familia. Kunahitajika hekima mpya na nguvu mpya, ili kukuza na kutetea ndoa, familia na maisha







All the contents on this site are copyrighted ©.