Baba Mtakatifu Francisco, hivi karibuni ataanza mfululizo wa ziara za Kimataifa ambamo
wiki ijayo ana ratiba ya kutembelea Korea Kusini kwa muda wa siku tano tangu tarehe
13-18 Agosti 2014. Aidha mwezi Septemba atakuwa nia ziara nyingine ya kitume nchini
Albania Septemba 21 , 2014, na anatazamia kutembela Sri Lanka kati ya tarehe 15-19
Januari 2015.
Katika ziara ya wiki ijayo kutembelea Korea Kusini , kati ya
shughuli muhimu zitakazofanywa na Papa katika ziara hii ni pamoja na kuongoza Ibada
ya Misa kwa nia ya kuwataja kuwa wenye Heri Watumishi wa Mungu, Paulo Yun Ji-chung
na wenzake 124, katika Ibada itakayofanyika katika uwanja wa GwangHwaMoon. Wafia dini
hao wanatajwa kuwa kizazi cha kwanza Wakatoliki Wakorea. Watoto wao tayari walitajwa
walikwisha pewa heshima ya kuwa wenye heri katika Ibada iliyofanyika mwaka 1984. Uwanja
wa GwangHwaMoon ni mahali pa kihistoria, na ni kituo cha mjini Seoul.
Historia
inataja Haemi ni mahali palipofanyika mauaji ya Wakorea 132, ambao wengi wao majina
yao hayajulikani, lakini walikamatwa na kuuawa wakati wakikimbilia Naepo kusalimisha
roho zao lakini walikamatwa na kuangamizwa kwa sababu ya kukiri imani yao kwa Kristo.
Baadhi ya wanafunzi walizikwa wakiwa hai wakati wa mateso ya Mujin 868.
Mahali
mauaji hayo yalipofanyika pamekuwa leo hii sehemu ya sala kwa kumbukumbu ya mateso
na mauaji ya waamini, pakijulikana kama kijiji cha Kkottongne ( Kijiji cha maua )
kilicho anzishwa mwaka 1976 na Padre Oh Woong Jin, ambaye aliamua kujenga "Nyumba
ya Upendo" baada ya kuona upendo wa kina wa muumini mmoja, Gwi Dong Choi, akitoa
chakula kwa watu maskini na walemavu wapatao 18. Padre Oh Woong Jin, aliguswa na huduma
hiyo na kuanzisha kituo rasmi cha kutoa msaada kwa maskini wasiojiweza , walemavu
, wasio kuwa na makazi na hata walevi wa kupindukia. Uzoefu wa Kkottongne ulivuka
mipaka , na kutawanyika katika mataifa mengine kama Bangladesh, Philippines, Uganda,
Haiti, India, Canada na Marekani.
Huduma hii muhimu katika kijiji hiki, hutegemea
michango na misaada kutoka kwa waamini na pia msaada wa serikali. Na kwa wakati
huu kinaendeshwa na Shirika la Masita wa Yesu wa Kkottongne wapatao 211. Pia kunaShirika
la Ndungu (Brothers)wa Yesu wa Kkottongne wapato 65, na husaidiwa na watu wa kujitolea
wapatao 1,000 ambao hupeana zamu kufanikisha shughuli za kijiji hiki ambach kwa sasa
kina uwezo wa kuhifadhi watu 5,000, watu waliopoteza tumaini , walemavu na waliotelekezwa
na familia zao. Kituo hiki cha Kkottongne pia hujulikana kama Nyumba ya Malaika kutokana
na huduma zake kuwa nzuri. Ndani ya kijiji mna shule ambapo watoto walemavu waliotelekezwa
na familia zao kwa sababu ya ulemavu wao huweza kujifunza kwa wakiwa 121.
Kardinali
Ferdinando Filoni, Mkuu wa shirika kwa ajili ya UInjlishaji mpya, anaielezea historia
ya Kanisa Katoliki Korea na upendo wake wa kimisionari udhahiri katika matendo ya
walei, yanayotoaa sura kamili ya Kanisa katika ujumbe wake wa kudumu, kama ilivyo
ainishwa katiak Waraka wa Kitume wa Papa Francisco, wa Fraha ya InjiliGaudium Evangelii.
Haya alieleza wakati wa na gazeti la “Vatican Insider"juu ya ziara ya Papa Francisco
hivi karibuni Korea ya Kusini, ambako Papa atawataja kuwa wenye Heri waamini 124,
waliouawa kwa kushupalia kikamilifu imani yao. Kardinali anaelezea kama mashahidi
hao wa imani , inakuwa ni ishara ya kutia moyo, katika kukumbuka pia kwamba, katika
nchi mbalimbali dunani , Papa ana nafasi yake. Na hivyo kuna matumaini kwamba , ipo
siku, Mkuu wa Kanisa la Ulimwengu pia ataweza kutembelea hata China.