Serikali ya Kenya imeamua kutaifisha asilimi 70% ya ardhi ya Lamu, eneo maarufu sana
kwa shughuli za utalii kutokana na mauzo yake kufanywa kinyume cha sheria. Uamuzi
huu umetolewa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya baada ya mashambulizi ya kigaidi kuzidi
kujitokeza kwenye mwambao wa Kenya na hivyo kusababisha maafa makubwa kwa watu na
mali zao.
Vyombo vya sheria nchini Kenya vimegundua kwamba, mashirika 22 ya
kigeni yamenunua ardhi eneo la Lamu kinyume cha sheria kati ya mwaka 2011 hadi mwaka
2012. Vitendo vya kigaidi vilivyowahusisha hata baadhi ya viongozi wa serikali za
mtaa pamoja na migogoro ya ardhi ni kati ya mambo ambayo yamechochea mashambulizi
kwa watu wasiokuwa na hatia.