2014-08-05 09:25:36

Bara la Afrika na haki msingi za binadamu!


Dr. Adelardus Kilangi, Mhadhiri wa Sheria za Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino cha Tanzania, SAUT ambaye pia ni Kamishina wa Sheria za Kimataifa katika Umoja wa Afrika katika mahojiano maalum na Radio Vatican anabainisha kwamba, utekelezaji wa haki msingi za binadamu ni kati ya changamoto kubwa zinazolikabili Bara la Afrika. RealAudioMP3

Bara la Afrika limezieleza na kuzifafanua haki msingi za binadamu kimataifa na kikanda mintarafu Tamko la haki msingi za binadamu la Umoja wa Mataifa; Mikataba ya haki msingi za binadamu ya mwaka 1966; Haki za binadamu katika muktadha na mazingira ya Bara la Afrika; kuundwa kwa Tume ya haki na amani ya Umoja wa Afrika pamoja na Mahakama ya Haki Barani Afrika. Mambo yote haya yanafahamika kwa viongozi wa Bara la Afrika, changamoto kubwa iliyoko mbele yao ni kuhakikisha kwamba, sheria hizi zinatekelezwa kikamilifu.







All the contents on this site are copyrighted ©.