2014-08-04 15:00:53

Papa aomboleza ya kifo cha Kardinali Clancy


Baba Mtakatifu Francisco amepeleka salaam za rambirambi kwa Askofu Mkuu Peter Comensoli , Mtawala wa kitume wa Jimbo kuu la Sydney Australia, kufuatia kifo cha Kardinali Edward Beda Clancy , kilichotokea majira ya saa tano za asubuhi Jumapili iliyopita.

Katika rambirambi hizo, Papa kwa moyo wa dhati wa kibaba, amesema, yupo pamoja na Askofu Mkuu Comensoli, na waamini wote wa jimbo kuu la Sydney. Na anaungana nao katika sala za kuiombea roho marehemu Kardinali Edward Clancy ipokelewe kwa Mungu, Baba wa rehema, kwa moyo wa shukrani kwa miaka yake ya huduma ya kiaskofu, na hekima zake za kichungaji kwa wakati wa uongozi wake katika Jimbo Kuu la Sydney, katika kujali mahitaji ya maskini,na msaada wake kwa ajili ya elimu Katoliki na kiekumeni na maono yake katika mtazamo mpana wa uraia.

Baba Mtakatifu ametoa baraka zake kwa wote , watakao shiriki katika Ibada ya Misa ya Wafu na Mazishi na wote wanao omboleza na kuguswa kwa namna ya kipekee na kifo cha Kardinali Clancy, waweze kuomboleza katika tumaini la ufufuo wa Kristo na ahadi ya uweza na faraja katika Bwana.








All the contents on this site are copyrighted ©.