Tovuti kwa ajili ya hija ya kitume ya Papa Francisko Korea ya Kusini
Baraza la Maaskofu Katoliki Korea hivi karibuni limezindua tovuti maalum kwa ajili
ya kuwasaidia waamini na watu wenye mapenzi mema wanaotaka kufuatilia kwa karibu zaidi
hija ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Korea, itakayoanza kutimua vumbi kuanzia tarehe
14 hadi 18 Agosti 2014. 00:01:54:84
Hii ni sehemu ya maadhimisho
ya Siku ya Sita ya Vijana Barani Ulaya inayoongozwa na kauli mbiu “Ondoka, uangaze,
kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia”, maadhimisho ambayo yatafanyika
Jimboni Daejeon, Korea ya Kusini. Kwa wale wanaopenda kufuatilia matukio haya wanaweza
kutembelea katika tovuti ifuatayo:
Tovuti hii inapatikana kwa lugha ya Kiingereza
na Kikorea. Mtandao huu una utajiri mkubwa wa habari, matukio yatakayokuwepo, liturujia,
sala na maana ya tukio hili la kihistoria. Nembo inayoongoza hija hii ya kitume ya
Baba Mtakatifu Francisko inachota utajiri wake kutoka katika maneno ya Nabii Isya,
“Ondoka, Uangaze”.
Nembo inaonesha mtumbwi na miale ya moto inayoiangazia dunia,
changamoto kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema Barani Asia na Korea kwa namna
ya pekee kutembea katika mwanga wa Bwana. Itakumbukwa kwamba, Baba Mtakatifu pia anatarajiwa
kuwatangaza Watumishi wa Mungu 124 kuwa Wenyeheri. Ibada ya Misa Takatifu kwa aliji
ya kuwatangaza Mashahidi hawa kutoka Korea, inatarajiwa kuadhimishwa hapo tarehe 16
Agosti, kwenye mji wa Guanhwamoon.
Baba Mtakatifu Francisko anafanya hija
hii ya kitume nchini Korea, ikiwa imekwisha kutimia miaka 25 tangu Mtakatifu Yohane
Paulo II alipotembelea Korea kunako mwaka 1989, ili kushiriki katika Maadhimisho ya
Kongamano la Ekaristi Takatifu Kimataifa.