2014-07-29 12:22:04

Papa kutembelea Sri Lanka na Ufilippini, Januari 2015


Baba Mtakatifu Francisko amekubali mwaliko uliotolewa na Serikali na Baraza la Maaskofu Katoliki Sri Lanka na hivyo, atatembelea nchini Sri Lanka kuanzia tarehe 12 hadi tarehe 15 Januari 2015.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amekubali pia mwaliko wa kutembelea nchini Ufilippini kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 19 Januari 2015. Taarifa inaendelea kuonesha kwamba, Vatican kwa siku za usoni, itatoa ufafanuzi zaidi wa hija hii ya kitume ya Baba Mtakatifu Barani Asia!







All the contents on this site are copyrighted ©.