2014-07-26 15:38:10

Vuteni subira, hakuna haraka!


Padre Federico Lombardi msemaji mkuu wa Vatican anafafanua kwamba, hadi sasa Baba Mtakatifu Francisko amepata mialiko mingi nchini Marekani na bado inafanyiwa kazi. Kuhusu ushiriki wa Baba Mtakatifu Francisko kwenye maadhimisho ya Siku ya Nane ya Familia kimataifa itakayoadhimishwa Jimbo kuu la Philadelphia, Marekani kunako mwaka 2015, Padre Lombardi anawasihi waamini kuvuta subira, watajulishwa kwa wakati muafaka!

Hadi sasa Baba Mtakatifu Francisko ameonesha utashi wake wa kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Nane ya Familia Kimataifa, lakini hadi sasa hakuna mchakato ambao umekwishaanzishwa kwa ajili ya safari hii ya kitume nchini Marekani au Mexico, kama ambavyo baadhi ya waandishi wa habari walivyotaka kufahamu. Bado kuna mwaka mzima, kabla ya tukio hili kuadhimishwa huko Philadelphia, Marekani!







All the contents on this site are copyrighted ©.