Askofu mkuu Souraphiel achaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa AMECEA
Wajumbe wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki
na kati, AMECEA katika mkutano wake wa kumi na nane uliokuwa unaongozwa na kauli mbiu
"Uinjilishaji kwa njia ya wongofu na ushuhuda wa imani ya Kikristo", wamemchagua Askofu
mkuu Berhaneyesus D. Souraphiel wa Jimbo kuu la Addis Ababa, nchini Ethiopia kuwa
Mwenyekiti mpya wa AMECEA. Askofu mkuu Souraphiel anachakua nafasi ya Askofu mkuu
Tarcisius Zizaye wa Jimbo kuu la Lilongwe, Malawi aliyemaliza muda wake.
Askofu
mkuu Souraphiel alipadrishwa kunako tarehe 4 Julai 1976. Akawekwa wakfu kuwa Askofu
kunako mwaka 1998 na kunako tarehe 7 Julai 1999 akateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo
kuu la Addis Ababa kwa kumrithi Kardinali Paulos Tzadua aliyekuwa analiongoza Jimbo
kuu la Addid Ababa, Ethiopia.