Baba Mtakatifu Francisko , mara baada ya kupewa taarifa za ajali ya ndege iliyoaguka
karibu na uwanja wa ndege wa Magong Taiwan, siku ya Jumatano, k alipeleka salaam
za rambirambi kwa familia zote za wahanga wa ajali hii. Na aliwahakikishia sala na
maombezi yake kwa ajili ya wote walioathirika na janga hili. Juu ya yote, anawaombea
baraka na faraja, nguvu na amani ya Bwana wa uzima wa milele.
Salaam hizi,
zilitumwa kwa niaba ya Papa na Kardinali Piero Parolin, Katibu wa Vatican, kwa Askofu
Mkuu John HUng Shan Chuan wa Jimbo Kuu la Tapei , na Rais wa Baraza la Maaskofu Kanda
ya China.
Jumatano ndege ya Shirika la Ndege la Taiwan, ikiwa na watu 58,
kati ya wakiwa wasafiri 54 na wafanyakazi wa ndege, ilianguka wakati ikijaribu kutua
ghafla katika uwanja wa Magong. Kati ya wasafiri hao 47 walifariki papo hapo na wengine
kunusulika ambao wengi wao hali zao zinatajwa kuwa ni mbaya . Chanzo cha ajali hiyo
ni hali mbaya ya hewa, iliyoandamana kibunga kikali, mvua kubwa na upepo mkali. Hali
iliyofanya hata shule na maeneo ya biashara katika mji huo kufungwa kwa muda. Ndege
hiyo ilikuwa katika safari zake za kawaida kati ya mji wa Kahohsiung na kisiwa cha
Penghu.