2014-07-22 15:16:10

Mkutano wa Maaskofu wa Lusophone-Angola


Kwa muda wa wiki zima kuanzia Jumatatu hii, Angola kwa mara ya kwanza itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Maaskofu Katoliki kutoka nchi zinazo zungumza Kireno (Lusophone). Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa juu ya mkutano huo na Baraza la Maaskofu la Angola, na Sao Tome, katika siku za kwanza za kikao hiki , Maaskofu watafanya vikao katika hali ya faragha , ambamo watajadili zaidi juu ya ajenda msingi za Mkutano. Na tangu Jumatano, majadiliano yatafanyika katika Chuo Kikuu Katoliki cha Luanda yakiwa wazi kwa umma.

Kati ya wanaohudhuria mkutano huu ni Kardinali Raymundo Damasceno Assis, Askofu Mkuu wa Aprecida na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Brazil , pia yupo Askofu Mkuu Manuel Josè Macàriòdo Nascimento Clemente Patriaki wa Lisbon. Mkutano huu hasa unalenga katika mada “ uwajibikaji wa Kiinjili katika kuibadili jamii kwa mwanga wa Waraka wa Injili ya furaha “Evangelii Gaudium “,wa Papa Francisko.

Aidha katika majadiliano hayo , Maaskofu pia watatazama mada zingine mbalimbali ikiwemo wajibu wa kanisa katika mahusiano na watu maskini katika mtazamo wa uchumi wa dunia na wajibu wa kanisa katika mapambano ya kisiasa duniani.

AskofuMkuu Gabriel Mbilingui wa Jimbo Kuu la Lubango na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Angola na Sao Tome , anasema, Mkusanyiko huu wa viongozi wa kanisa kutoka nchi zinazozungumza kireno , ni jukwaa la kushirikishana uzoefu na changamoto katika kufanikisha kazi ya kuhubiri Injili ya upendo na ufanikishaji wa maisha chanya kwa jamii inayozungumza Kireno.

Mataifa yanayozungumza Kireno yaliunda jukwaa hili la nchi za Lusophoni, mwaka 1996. Nchi zinazohusika ni Angola, Sao Tome na Pricipe Guinea Bissau, Musumbiji, Ureno, Capo Verdena Brazil pia Timor ya Mashariki . Mkutano huu umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka miwili kwa lengo la kujenga uhusiano wa karibu zaidi .

Ijumaa 25 Julai , Maaskofu watakwenda Benguela ambako watakutana na jumuiya mbalimbali . Na Jumapili 27 Julai watajumuika pamoja na waamini katika maadhimisho ya Ibada ya Misa.

Rais wa Jamhuri ya Angola , ameutaja mkutano huu kuwa ni mkutano chanya kwa utendaji wa kimbinu kwa ajili ya manufaa ya jamii inayozungumza Kireno, watu wapatao millioni 223 waliotanyika sehemu mbalimbali za dunia. . Makao makuu ya Lusophoni yako Lisbon Ureno.








All the contents on this site are copyrighted ©.