2014-07-22 15:01:57

Jumamosi, Papa Francisko, anautembelea mji wa Caserta Italia.


(Vatican Radio) Jumamosi ya wiki hii, Papa Francisco, ana ratiba ya kutembelea mji wa Caserta, Kusini mwa Italia, ambako atakutana na viongozi wa Makanisa , Katoliki na Kiinjili ya eneo hilo.

Maelezo yaliyotolea siku ya Jumatatu juu ya safari hii yanasema, alasiri Jumamosi 26 Julai, Papa atatumia usafiri wa helikopta hadi katika mji huo, ambako atakuwa na mkutano na viongozi wa dini, ikifuatiwa na Ibada ya Misa katika eneo la wazi, maarufu linalojulikana kama Reggia di Caserta.

Baba Mtakatifu mara baada ya kukamilisha ratiba ya Jumamosi jioni, atarejea Vatican. Lakini siku ya Jumatatu 28 Julai, anarudi tena katika mji huo ambako atakuwa na ziara binafsi ya kukutana na kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Upatanisho Mchungaji Giovanni Traettino. Mchungaji Traettino, walijenga urafiki tangu miaka ya nyuma, wakati Papa akiwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires. Na kwa pamoja walishiriki katika matukio ya kiekumeni kwenye eneo lao, yaliyojumuiya wanaharakati wa Uamusho mpya wa Kiroho ndani ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili.

Kwa wakati huo, Kardinali Jorge Bergoglio, pamoja Mchungaji Giovanni Traettino na Padre Raniero Cantalamessa, mhubiri wa kaya ya Papa, walikuwa wasemaji wakuu Kwenye mkusanyiko huo wa kiekumeni. Mikutano unaotajwa kuwa mkubwa wa aina yake uliofanyika katika mji mkuu wa Argentina mwaka 2006. Mwezi uliopita, Papa alikutana faragha na kundi la Wachungaji Kanisa la Kiinjili na Wainjilisti katika makazi yake ya Vatican.


AskofuGiovanni D'Avise wa Jimbo Katoliki la Caserta, ameiambia Vatican Radio, baada ya habari hii kutolewa rasmi, kwamba, ingawa wamekuwa na kipindi kifupi cha kufanya maandalizi kwa ajili ya ujio wa Papa, watu jimboni mwake wameonyesha moyo wa furaha na shukurani kwa kutembelewa na Papa. Na kwamba , maadhimisho ya Ibada ya Misa, yatafanyika sambamba na sherehe ya Sikukuu ya Mtakatifu Anne, Mama wa Bikira Maria na pia ni ishara nzuri ya kuimarisha ushirikiano wa viongozi katika mji wa Caserta.








All the contents on this site are copyrighted ©.