2014-07-22 09:28:18

Cheche za amani ya kudumu nchini Senegal


Jumuiya ya Mtakatifu Egidio yenye Makao yake makuu mjini Roma, inaendelea kufuatilia kwa kina na mapana mkataba wa kusitisha mapigano ili haki, amani na upatanisho viweze kushika mkondo wake tena nchini Senegal. RealAudioMP3

Hivi karibuni, ujumbe wa Serikali ya Senegal na Chama cha Upinzani cha MFDC, umetembelea Makao Makuu ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na kujadiliana kwa pamoja mikakati iliyoainishwa tarehe 3 Novemba 2013 kuhusiana na masuala ya kibinadamu. Wajumbe wa pande hizi mbili wamejadili na kuchangia uzoefu na mang’amuzi na kwamba, kwa sasa wanaaminiana zaidi.

Kwa pamoja wajumbe wameonesha utashi wa kushirikiana ili kuyapatia ufumbuzi matatizo na shida zinazowasibu wananchi wa Senegal kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa miaka kadhaa nchini humo. Wajumbe wameridhia waraka watakaoufanyia kazi na kuridhiwa kwa ukweli, uwazi, upendo na mshikamano, kanuni msingi zilizoongoza majadiliano ya kuendelea kuimarisha amani, mshikamano na upatanisho wa kitaifa.

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imefurahishwa na mafanikio yaliyokwishakufikiwa hadi sasa na kwamba, inatumaini kuwa pande hizi mbili zitaweza kufikia muafaka wa amani na amani ya kudumu.








All the contents on this site are copyrighted ©.