2014-07-21 08:57:51

Kamwe vurugu haiwezi kuondoa vurugu!


Vatican Radio) Jumapili Papa Francis alionyesha kuhofia hatma ya jamii ya Kikristo katika mji wa Mosul Iraq ,na katika sehemu nyingine za Mashariki ya Kati, ambako kwa wakati huu kuna mapambano makali ya vita vya wenyewwe kwa wenyewe.

Akizungumza baada ya sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Papa aliyaelekeza mawazo yake, kwa Wakristo wanaoteseka katika nchi yao, ambayo wamekuwa wakiishi tangu mwanzo wa Ukristo, akisema ni sadaka yenye mchango thamani sana kwa manufaa ya jamii zima ya biandamu.

Wakristo hao, ndugu zetu wanateswa! Hao wametengwa na nyumba zao na kulazimishwa kukimbia bila hata kuwa na uwezo wa kuchukua mali zao, alieleza kwa masikitiko na kuwahakikishia ukaribu wake na sala za mara kwa mara. Pia alionyesha kutambua mateso ya wake kwa waume, akisema anafahamu kwa jinsi gani wanateseka , na kwamba kiimani anateseka pamoja nao hadi hapo katika Jina la Bwana, uovu utakaposhindwa.


Kisha Papa alitoa wito kwa wote, tangu wale waliokuwa wakimsikiliza katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hadi kona zote za dunia, wadumu katika kuomba kwa ajili ya amani katika hali zote za mivutano na migogoro duniani , na hasa Mashariki ya Kati na Ukraina. “Mungu wa amani, na aamushe hamu halisi kwa ajili ya mazungumzo na maridhiano. Kame vurugu haiwezi kuondoa vurugu. Vurugu ni kujitenga mbali na amani”!

Papa alitoa wito huu, baada ya kutafakari somo la Injili la Jumapili , ikifuatia na sala ya Malaika wa Bwana. Kwa ajili ya tafakari kwa somo la Injili ya siku, Papa alieleza maana ya mfano wa mpanzi uliotajwa katika Injili, mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake na adui yake usiku kumpandia magugu. Na wakati watumishi wa shamba walipotaka kuyatoa magugu mapema, bwana wao aliwakataza akisema, watang’oa pia mizizi ya ngano na hivyo ni vyema kuacha vyote kukua pamoja, ngano na magugu.

Mfano huu - Papa Francisco alielezea – ​​unazungumzia wakati wetu huu, ambamo watu wema wanaishi na matatizo ya maovu duniani na inaonyesha uvumilivu wa Mungu.

Shetani , anapanda mbegu ya maovu ambako kuna mbegu nzuri ya wema, anajaribu kuwagwwa watu , familia na mataifa. Lakini Mungu anajua jinsi ya kusubiri. Mungu anatazama katika 'shamba' la kila mtu kwa uvumilivu na huruma: anaona uchafu na uovu vizuri zaidi kuliko sisi, lakini yeye pia anaona mbegu za nzuri na kwa uvumilivu anasubiri ziote na kukomaa.

Mungu - Papa Francis alisema - ni Baba Mvumilivu mwenye kusubiri kwa moyo wazi wa kuwakaribisha wenye kumkosea na husamehe makosa yetu bila kuchoka. Lakini uvumilivu wake hauna maana kwamba hakichukizwi na maovu. Yeye daima hachanganyi mema na mabaya. Na mwisho, wakati wa mavuno, Yesu atatoa hukumu kwa wote, kuwatenganisha wale ambao ni mbegu nzuri kutoka kwa wale ambao ni mbegu ya magugu. Na hivyo Papa ameonya, tutahukumiwa kwa kipimo hichohicho tunachotumia kuwahukumu wengine, na ni huruma hiyohiyo tutakayopewa ambayo sisi pia tunaionyesha kwa wengine.
Papa alimalizia kwa kuomba msaada wa Mama yetu Maria , atusaidie kukua katika uvumilivu na katika huruma.








All the contents on this site are copyrighted ©.